MWENYEZI MUNGU ATUHADHARISHA KUHUSU FITINA ZA MAWAHHABI (ANSWAR SUNNAH au MASALAFI)

Katika Qur’an, Surat Anfaal aya ya 25, Mwenyezi Mungu anatuambia kuwa, “Na Jikingeni na fitina ambayo haitowasibu wale waliodhulumu miongoni mwenu peke yao, na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali ya kuadhibu”.
Ufafanuzi: Fitina na Mauaji yanayofanywa na Mawahhabi inawauwa waislamu zaidi kuliko madhalimu. Chukua daftari na andika orodha ya watu wanaolipuliwa na Mawahhbi, utakuta kuwa wanaouwawa kwa asilimia 99 ni waislamu. Ni akina nani wanauliwa na Boko Haram, Alqaida, Jabhat Annusra na Mawahhabi wengine huko Nigeria, Pakistan, Iraq, Syria, Yemen, Somalia, Mali, Libya, n.k. wanaochinjwa huko ni waislamu. Hii ndio sababu Allah (s.w) akatuonya kuhusu udhalimu wao.
Mtafsiri mkuu wa Qur’an ni Mtume Mohammad (S.A.W), na hakubaki nyuma katika kuitafsiri aya hii (8.25) kwa hadith ifuatayo:
Fitina itatoka Mashariki (Najdi), huko litachomoza pembe la shetani.
Rejea:
1. Sahihi Bukhari, Juzuu ya 1 – 4, kitabu fitan, hadith namba 1037, 3104, 3279, 3511, 5296, 7061, 7092, 7093, 7094
2. Sahihi Muslim, Babul fitna minal Mashariki min haithu tatuluu qarna shaytwan, hadith namba 2905 kifungu cha 45, 46,47, 48, 49, 50

Comments