Yeye ni Muhammad bin Abdul-Wahhabi bin Suleiman bin Ally bin Muhammad bin Ahmed bin Rashid wa kabila la Watamimu. Alizaliwa mwaka 1703 miladia katika mji wa Uyaynah katika nchi ya Najdi. Kuna hadith nyingi za Mtume Mohammad (S.A.W.W) zinazowazindua waislamu juu ya fitina na balaa za upotovu utakao tokea katika dini kwa kuletwa na Mohammad Abdul-Wahhabi.
Wanazuoni wengi wamehakikisha kuwa hadith hizo zilikuwa zinamtabiri Muhammad Abdulwahhabi na wazushi wengine kama Musaillama Al-Kadhab ambaye ni babu wa mababu wa mfalme Mohammad bin Saud aliyeasisi ufalme wa Saudi Arabia kwa kushirikiana na sheikh mpotofu Mohammad Abdulwahhabi wakiongozwa na serikali ya Uingereza.
Amesema Mtume Mohammad (S.A.W.W) kuwa atakuja tokea shetani kutoka Najdi, litatikisika Bara Arabu kutokana na fitina zake.

Katika hadith nyingine Mtume wetu amesema kuwa itatokea fitina kutoka huko, kutoka huko, (huku akiashiria kwa mkono wake mtukufu upande wa Mashariki yaani Najdi).
Katika Sahihi Muslim, katika hadith iliyopokelewa na Abihuraira, Mtume (S.A.W.W) amesema, “kichwa cha kufru ni (kutoka) Mashariki”, ambako ndiko iliko Najdi alikozaliwa Mohammad Abdul-Wahhab.
Siku moja Mtume alikuwa akiomba dua kama ifuatavyo, “Ewe Mola wangu tubariki katika Shamu na Yemen”. Wakasema (watu wa Najdi iombee) na Najdi yetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume akakariri dua hiyo mara tatu akiiombea Shamu na Yemen na hali wao watu wa Najdi wakisema iombee Najdi. Mara ya nne Mtume akasema huko (Najdi siombei) ni mahala pa misukosuko na fitna.
Hadithi zote hizo ni utabiri wa Mtume Mohammad (S.A.W.W) kuhusu fitna na hujuma zitakazofanywa na Mohammad Abdulwahhabi na wafuasi wake dhidi ya waislamu na wanadamu kwa ujumla. Chunguza waislamu kwa makini, ukikuta muislamu anayeshabika kuwakufurisha waislamu wengine na kuhimiza mauaji dhidi ya wanadamu, basi huyo ni mfuasi wa ibn Abdulwahhabi hata kama yeye mwenyewe akisema kuwa sio mhabiya. Uwahhabi ni tabia si lazima useme mimi ni muwahhabi bali tabia yako inatosha kukutambua kuwa ni muwahhabi. Je, hakuna watu wanaoshabikia farka na fitna baina ya waislamu, kisha wakawakufurisha waislamu wenzao? Basi hao ni mawahhabi.

Comments
Post a Comment