Neno Shia limetokana na neno la kiarabu Attashayyu, lenye maana ya kufuata. Kulingana na al-Qamus na Lisanul 'Arab, marafiki na wafuasi wa mtu wanaitwa Shia wake. Neno hili hutumika hivyo kwa umoja na kwa wingi, kwa wanaume na wanawake. Kamusi za kiarabu zinapotoa maana ya neno Shia, kwa kawaida huongeza maneno haya; jina hili kiujumla hutumika kwa wale wenye mapenzi na kumfuata Imam Ali (a.s) na watu wa nyumbani kwake, (yaani Ahlulbayt Nabii) na limekuwa ndio jina lao makhsusi (Al-Qamus, juzuu ya 2, na annihayah juzuu ya 2 uk. 519-520).
Katika Qur'an tukufu neno Shia limetumika kwa wafuasi wa mitume wa Allah:
a) Katika kisa cha nabii Mussa (a.s), Qur'an (28:15) inasema kuwa, “Huyu ni katika Shia wake, na yule ni katika adui zake, yule ambaye alikuwa Shia wake alimuomba msaada juu ya yule adui yake ...”
b) Katika kisa cha nabii Nuhu (a.s), Qur'an (37:83) inasema kuwa, “Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi (Shia) wake.
Sheikh al-Mufid ameeleza kuwa, wakati neno hili linapoanza na al- yaani al-Shia inamaana ya kundi pekee lenye kumfuata Imam Ali (a.s) kwa mapenzi na imani (itikadi) ya kwamba alikuwa ni imam na khalifa baada ya Mtume kufariki tu bila kuachwa mwanya wowote hata wa saa moja. (Awaili l-Makalatat uk 2-3).
kwa ufupi Shia wamepata jina hili kwa sababu wanamfuata Imam Ali (a.s) na kizazi chake walio Maasumin, na kuyapuuza madai ya watu wengine ya Ukhalifa au Uimam. Ni Mtume mwenyewe ndiye aliyewapa watu hawa jina hili (yaani Shia wa Ali).
Comments
Post a Comment