NISABU YA NG'OMBE (KIWANGO CHA KUTOLEA ZAKA)

NISABU YA NG'OMBE (KIWANGO CHA KUTOLEA ZAKA)
Ng'ombe wakiwa chini ya 30 hawatolewi Zaka.
Kutoka 30 mpaka 39 atatolewa ndama mmoja wa umri wa mwaka mmoja. kutoka 40 mpaka 59 atatolewa ndama mmoja wa umri wa miaka miwili. Kutoka 60 mpaka 69 watatolewa ndama wawili wa umri wa mwaka mmoja mmoja. Kutoka 70 mpaka 89 atatolewa ndama mmoja wa umri wa mwaka mmoja na ndama mmoja
wa umri wa miaka miwili.


Kutoka 90 mpaka 99 watatolewa ndama 3 wa umri wa mwaka mmoja mmoja. Kwa ng'ombe 100 watatolewa ndama 2 wenye umri wa mwaka mmoja na ndama mmoja mwenye umri miaka 2. Wakizidi hapo ndama mmoja wa umri wa mwaka mmoja atatolewa kwa ng'ombe 30 na ndama mmoja wa umri wa miaka miwili kwa ng'ombe 40. Ng'ombe wanaofanya kazi shambani hawahesabiwi pamoja na wale wanaotozwa Zaka.

Comments