Sisi kama Waislamu, hatufuati amri yeyote
ile ila sharti iwe imenasiwa katika Qur'ani ama katika Hadithi tukufu za Mtume
wetu (s.a.w.)
Saumu katika Qur'ani imetajwa kutoka Aya
ya 183 ya Sura ya pili 'ALBAQARAH' hadi Aya ya 187 ya Sura hiyo hiyo. Na
Mwenyezi Mungu Ametufunza kama ifwatavyo:
"Enyi mlioamini, mmelazimishwa
kufunga Saumu kama walivyolazimishwa wa kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezi
Mungu."
"Ni siku chache tu (zinazohesabiwa)
lakini miongoni mwenu awaye mgonjwa au katika safari, basi atimize hesabu
katika siku zingine. Na wale wanaoweza, watoe fidia kwa kumlisha masikini. Na
atakayefanya wema kwa radhi ya nafsi yake basi ni bora kwake, na mkifunga ni
bora kwenu mkiwa mnajua."
"(Mwezi mnaoambiwa kufunga) ni mwezi
wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa mwongozo kwa watu na ishara
silizo wazi za mwongozo na kipambanuzi. Basi miongoni mwenu atakayeuona mwezi
(au atakayekuwa mkazi asiwe msafiri pindi mwezi ufikapo) afunge Saumu na mwenye
kuwa mgonjwa au safarini basi atimize hesabu katika siku zingine. Mwenyezi
Mungu Huwatakieni mepesi wala Hawatakieni yaliyo mazito, na kamilisheni hesabu
na kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwaongozeni na ili mpate kumshukuru."
"Na waja wangu watakapokuuliza juu
yangu basi hakika Mimi nipo karibu, Nayaitika maombi ya mwombaji anaponiomba,
basi waniitikie na waniamini ili wapate kuongoka."
"Mmehalalishiwa usiku wa Saumu
kuwaingilia wake zenu, wao ni nguo kweni na nyinyi ni (kama) nguo kwao,
Mwenyezi Mungu amejuwa kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwa hivyo
amewakubalieni toba zenu na amewasameheni, basi sasa changanyikeni nao (yaani
laleni nao) na takeni aliyowaandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni mnyweni mpaka
ubainike kwenu uzi mweupe katika uzi mweusi wa Alfajiri, kisha timizeni Saumu
mpaka usiku, wala msitangamane nao
na hali mnakaa itikafu misikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu basi
msiikaribie. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyobainisha hoja zake kwa watu ili
wapate kumcha."
Maneno hayo ufasaha usioweza kukabiliwa na
mfasaha yeyote, ndiyo asili na misingi ya Saumu. Yeyote abishanaye au kukaidi
Amri tunamjibu hii basi huwa sio Mwislamu na bila shaka marejeo yake ni Jahanam
ambapo ni mahala pabaya kabasa. Jahanamu ambayo imeandaliwa kwa ajili ya watu
wasiomwamini mwenyezi Mungu, wale wapingao amri zake (makafiri) na washirikina,
yaani wale wanaomwabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kwa mfano wakristo
wanaomwabuni Yesu na Mama yake wakiwa vyeo lukuki kama vile Mungu mkuu, Mungu
mwana, Mama wa Mungu n.k. Haya ni makosa ambayo wanatakiwa watubie haraka kabla
ya siku ya mwisho ili waweze kupata amani ya milele kama sisi waislamu.
Comments
Post a Comment