SHAHADA YA MTOTO MCHANGA WA IMAM HUSSEIN ALI AL ASGHAR HUKO KARBALA:

Katika hali ya kuwadhalilisha watoto na familia ya mtume saww kwa sunna ya Yazeed L.A. kulitokea mengi katika seyra ya mjukuu wa Mtume Saww Imam Hussein A.S. na hii ni sunna ambayo mpaka sasa inaendelea duniani kutoka kwa maulamaa mpaka kwa watu wa kawaida. Hata yazid alikuwa akivaa kanzu kama waislam, hata shimr vile vile lakini roho zao zilikuwa mbali na quran na mafundisho ya bwana mtume saww. Heshima ni ya “lip service” au kwa mdomo tu.
Imam Hassan A.S anaeleza daraja yao kihivi:
من عرفني فقد عرفني ومن لم يعرفني فأنا : الحسن بن علي ثم تلا هذه الآية قول يوسف) ع) : وإتبعت ملة آبائي إبراهيم وإسحاق ويعقوب ، ثم أخذ في كتاب الله ، ثم قال : أنا إبن خاتم النبيين ، وأنا إبن البشير النذير ، وأنا إبن الداعي إلى الله بإذنه ، وأنا إبن السراج المنير ، وأنا إبن الذي أرسل رحمة للعالمين ، وأنا من أهل بيت الذي أذهب الله عنهم الرجس وطهرهم تطهيرا ، وأنا من أهل بيت الذين كان جبريل (ع) ينزل فينا ويصعد من عندنا.وأنا من أهل بيت الذين فرض الله تعالى مودتهم على كل مسلم. وأنزل الله فيهم : قل لا أسئلكم عليه أجراً إلاّّ المودة في القربى ، ومن يقترف حسنة نزد له فيها حسنا ، وإقتراف الحسنة مودتنا أهل البيت.
Yeyote anayenijua amenijua, na yule hanijui basi mimi ni Al- Hassan mtoto wa Ali, halafu akakariri aya ya Nabii Yusuf alivyojitambulisha.. “Na nikafuata mila ya babangu Ibrahimu na Ishaaq na Yaaaquub”, halafu akasema, mimi ni mwana wa nabii wa mwisho na mimi ni mwana wa mtoa habari njema muonyaji, na mimi ni mwana wa msemaji wa Allah kwa idhni yake na mimi ni mwana wa taa iliyo na mwangaza mwingi na mimi ni mwana wa yule aliletwa kama rahma kwa ulimwengu na mimi ni katika Ahlul Bayt ambaye alitakaswa kutokana na uchafu na kutwahirishwa na mtakaso maalum. Na mimi ni ahlul bayt ambapo Jibril A.S. alikuwa akija nyumbani kwetu akitushukia na akipanda kwetu. Na mimi ni katika Ahlul Bayt ambaye mumefardhishwa mapenzi juu yetu kutoka kwa kila muislamu na hata mwenyezi mungu aliteremsha ayah... Sema: siwaulizi ujira wowote ila mapenzi kwa aqrabu zangu na yeyote anaye fanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye shukrani na Mwenyezi Mungu Swt aliamrisha mapenzi juu yetu Ahlul Bayt.
(tafsiri ya ki juu juu )
Na pia kwa hadith ya thaqalayn mtume saww akisema:
“Ninakuachieni vitu viwili vizito (vyenye thamani) miongoni mwenu. Kwa kadiri mvifuatavyo vyote viwili hamtapotea. Vitu hivi viwili vyenye thamani ni Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na dhuria yangu Ahlul-Bayt.”
Kurudia mada ya karbala juu ya utovu wa nidham dhidi ya dhurriyya ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtume Saww ambapo amri ya mtume saww kuhusu itrah yake ahlul bayt kushikamana nao, kundi ovu lilifika “climax” yake kwa kudharau na kutupililia mbali wasia wa Quran na Hadith nyingi sana za mtume wao kuhusu kushikamana na Quran na Ahlul Bayt wake na badala ya hivyo wakatangaza kuwa kundi la ahlul bayt ni makafiri.
SHAHADA YA MTOTO WA MIEZI SITA ALI AL ASGHAR A.S.
Kundi la imam hassan lilikatazwa maji na majeshi ya khalifa wa sita wa kiwahabi yazid ibn muawiya. Watoto walilia kwa kiu na wanawake wakakosa maziwa ya kunyonyesha watoto wao akiwemo ali al asghar ambaye alikuwa mtoto wa Imam Hussein A.S.
Uzuiaji wa ugavi huu wa maji ulisababisha ukali zaidi wa kiu iliyohisiwa na HUSSEIN na watu wa kundi lake. Kuongezea fedheha kwenye jeraha hili, maadui wakati mwingine wakimhutubia HUSSEIN, wakisema, “Hapa pana maji, NA mbwa na nguruwe wanayanywa, punda na hata mbwa mwitu wanayatumia, lakini wewe na kundi lako hamtapata hata tone moja la maji hayo.”
Imam Hussein A.S. alimwomba mkewe Rubab A.S. ruhusa ya kumchukua mtoto wake mchanga Ali Al Asghar kuwaonyesha jeshi la batwil hali ya huyu mtoto ili apatiwe maji lau kidogo. Basi Imam Hussain A.S. akamnyanyua yule mtoto mchanga wake wa miezi sita akimwangalia jinsi kukosa maji kumemuathiri macho yameingia ndani na midomo imekauka. Kilio cha mtoto hakikua na nguvu tena. Imam hussein akambeba kuwaonyesha athari ya kiu cha kifo kilichowakumba na zaidi huyu mtoto asiyekuwa na dhambi.
Akamfunika na akaenda nayeye kwenye jeshi la Yazeed Mwana Wa Muawiya L.A. akamfunua Ali Al-Asghar A.S. huku akisema: “HUYU MTOTO HAJAFANYA DHAMBI LOLOTE, ANAKUFA KWA KIU. NAOMBA MATONE YA MAJI KIDOGO TU ILI NIMNYWESHE”.
Jeshi likapigwa na butwaa na kimya kikatanda kwa kishindo. Imam kwa sauti ya rehema na utulivu akamwambia mwanae Ali Al Asghar A.S.,
“Asghar mwanangu, waonyeshe unavyosikia kiu”,
Asghar akageuza kichwa chake kitukufu kuwaangalia wanajeshi wa Yazeed L.A.na akatabasamu, na akafungua kinywa chake kidogo na akatoa ulimi wake uliokuwa mkavu. Akauzungusha kinywani mwake huku wanajeshi wanaangalia.
Wallahi lilikuwa tukio la kuhuzunisha sana na Kundi katika jeshi la Yazeed waliokuwepo hapo walishindwa kustahimili na walisikika wakilia kwa kwikwi huku wakitokwa na machozi wakimuangalia huyo mtoto mjukuu wa kiumbe bora duniani Mtume Muhammad Saww aliyewaletea hii dini ambayo wanaoifuata na ghafla itrah yake au kizazi chake kinateswa kwa kurudi kwa ujahiliyya kwa waislamu. Binadamu wa kweli hawezi ila kuathirika na tukio kama hili. Mtoto anachezesha ulimi wake kwa mdomo mkavu akitamani maji na bado alikatazwa Majeshi wote walikuwa ni waislamu. Wote walimuamini Allah swt na mtume muhammad saww na wote waliitakidi kuwa muhammad saww ndiye mtume wake na wengine walisikia mtume akisema nawatahadharisheni na ahlul bayt wangu akawa anasema kila mara kabla ya kuaga dunia.
Mtume saww alikuwa amesema:
“Huenda nikaitwa na (Mola wangu) nami nikajibu, nami ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooshwa kutoka mbinguni hadi ardhini nacho Kizazi changu ni Ahlubait wangu (watu wa karibu wa nyumbani kwangu). Naye Mwingi wa huruma Aliyemjuzi wa yote amenijulisha kwamba havitotengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni mtakavyovitendea baada yangu”.
Imam hussein akaendelea kuwaambia, kama munaona mimi nitajinywesha mimi mwenyewe basi nitawaachia huyu mtoto hapa mumnyweshe wenyewe maji. Wakakataa.
Basi jawabu ya Imam Hussein kumleta mtoto wa huyu wa miezi sita Ali Al Asghar A.S. lilikuwa hili:
Umar Ibn Saad ambaye alikuwa kamanda wa jeshi la yazeed (huyu umar alikuwa ni mtoto wa sahaba Saad Ibn Abi Waqqas) mwenyezi mungu amlaani akafanya wasiwasi sana jinsi ushindi ulikuwa unaanza kupatikana kupitia kwa Ali Al-Asghar na wanajeshi wengine wameanza kupata huruma. Umar huyu l.a. akamwambia Harmala l.a. ambaye alikuwa ndiye mwenye shabaha zaidi ya kurusha mishale akaamuru hapo hapo
“ Mnyamazishe Hussein!! Mnyamazishe Hussein!!”.
Hapo hapo Harmala L.A. aliinua mshale wake na akalenga bila ya kukosea mshale ambao si wa ncha moja wala mbili bali mshale wa ncha tatu ambao hutumika kuua ngamia,. na imam akauona mshale unakuja akajaribu kuuzuia umuingie yeye lakini ukamdunga yeye na ukasafiri mpaka kwa shingo ya Ali Al Asghar na hapo hapo huyu mtoto akaaga dunia na kupata busu la ushahidi huku akiwa mikononi mwa babake.
Allah akbar allah akbar
Imam Hussein A.S. alishika ule mshale akajaribu kuung’oa pole pole ili mtoto asihisi uchungu mwingi lakini ikawa ameaga dunia pale pale. Fikiria mtoto mdogo wa miezi sita wako au wa ndugu yako amepigwa mshale mikononi mwako na umezingirwa na maadui. Imam hussein alitaka Damu iliyomwagika kwenye shingo ya huyu mtoto kuirusha juu mbinguni au kuimwaga kwenye ardhi akabadili nia na akajipaka damu ya huyu mtoto usoni mwake akihofia hakungenyesha mvua hiyo sehemu tena masiha na hakuna mimea ingemea hapo mahala tena. Ndipo akaamua kujipaka hiyo damu ya kitukuu cha habib al mustafa saww.
Imam A.S. akaangalia juu huku akiomba” Ya Allah nipe ujasiri katika wakati huu mgumu katika maisha yangu.akataka kurusha hiyo damu juu mbinguni akasikia sauti inamwambia ..la hussayn usirushe juu ama hakutawahi kunyesha mvua sehemu hii tena maisha. Na alipotaka kumwaga chini aksikia sauti anaambiwa ardhi inaogopa kupokea damu tukufu. Ndipo akaamua kujipaka hiyo damu ya kitukuu cha Habib Al Mustafa Saww.
Imam a.s. akashindwa atamwambiaje mamake kilichotokea. Nguvu zilimwisha imam hussein Akaenda katika hema la mamake Ali Al Asghar A.S. Hadhrat Umm Rubab A.S. alipokuwa anakaribia, akashindwa kuingia moja kwa moja.
Alipofika kwa hema akarudi nyuma na akapiga hatua 7 nyuma. Akasema kwa sauti ya huzuni ... Inna Lillah Wainnaa Ilayhi Raajiuun..... akaenda tena pale kwa hema akawa anashindwa ataanza vipi kutoa habari ya kifo cha huyu mtoto kwa mamake. Alipofika akarudi hatua saba tena nyuma huku akisema Inna Lillah Wainna Ilayhi Raajiuun.
Imam Hussein A.S. alifanya hivi MARA SABA (7) huku akishindwa atatoa habari hizi za kuhuzunisha vip kwa mama mtoto. ndipo mwishowe Imam akaenda kwa mama mtoto Umm Rubab Ya Allah, A.S. na yule mtoto akasema : Rubab! Njoo umchukue mwanajeshi wako mdogo aliyekufa fy sabiilillah. Mama mtoto akamkumbatia baba mtoto analia kupita kiasi na kushindwa kujizuia hajui asikitike kivipi. Imam akamwambia, “Huu ni mtihani kutoka kwa Allah ambao hakuna mama ashawahi kupewa. Twende tumzike”.
Basi imam akamchukua mtoto kwa mamaye akamwambia acha tumzike mara moja. Imam akachimba kaburi dogo na upanga wa Bwna Mtume Saww aliompa imam ali a.s. , upanga Dhul Fiqaar ambao mtume saww aliusifu kusema uislamu haungeenea bila ya mali ya bi khadija na upanga dhul fiqaar ya imam ali a.s.
Je ushawahi kumchimbia mwanao kaburi na ukamzika katika uwanja wa vita na mama yake. Hichi ndicho kizazi cha mtume wenu kilivyofanywa baada ya babu yao kuaga dunia. Ukabaila na ukabila wa kijahiliyya ambao ulikuwa haujatoka kwa makabila fulani na chuki ya mababu zao waliouliwa badr na uhud bado ulikuwa unawaka moto kwa wajukuu wao khususan kabila la Banu Umayya walioona huu ndio wakati muafaka wa kulipiza kisasi dhidi ya Banu Hashim waliokirimiwa na Allah swt kwa kupewa utume na fadhila nyingi juu ya wengine. Hakika allah swt anachagua atakavyo na sisi hatuna amri kwa Allah swt kwani hufanya atakavyo
Mtoto huyu kaburi lake liko pale pale katika uwanja wa Karbala. na kaburi hili dogo la ali al asghar halikupata maji kunynyunyiziwa ila machozi ya imam husseyn na watu wake.
Inna lillah wainna ilayhi raajiuun.
ASSALAMU ALAIKA YA RADHWI3 Al-SWAGHIIR
ASSALAMU ALAYKA YA ALI AL ASGHAR WARAHMATULLAHI WABARAKAATUH

Comments