Swali: Je!! Uimamu na ukhalifa ni uteuzi wake Mwenyezi Mungu au ni uteuzi wa Watu?

Jibu: Uimamu na ukhalifa uteuzi wa imam na khalifa ulifanywa na mtume mtukufu (s.a.w.w.) kutokana na agizo la Mungu peke yake. kwa hiyo hakuna imkani yoyote ya kuwahusisha watu katika uteuzi huo. mwenyezi mungu amesema katika qur'an: "na ni mola wako huumba na kumteua atakavyo viumbe hawana hiari katika jambo hili. mwenyezi mungu ameepukana na kasoro, na ametakasika na hao wawashirikishao (naye)" (28:68). katika qur'an tukufu allah amewateua manabii adam na daudi kuwa makhalifa tu; wawakilishi wake duniani "eh daud bila shaka nilikuteua uwe mtawala juu ya ardhi". (38:26). hata hivyo licha ya kumteua awe nabii na khalifa vile vile alimpa hadhi ya kuwa imam". kwa hakika mimi nitakufanya wewe imam". (2:124).

kutokana na hadithi mashuhuri ya mtume (s.a.w.w.), watakuwa warithi kumi na wawili baada yake. wanazuoni mashuhuri wa madhehebu ya kisunni wameukubali ukweli wa hadithi hiyo na kunakili katika vitabu vyao. vile vile katika historia ya kiislam, banu ummaya, na banu abbasi walikuwa watawala wa kidunia tu, wao kamwe hawakuteuliwa na mtume mtukufu (s.a.w.w.). kwa hakika kufuatana na hadithi zingine, mtume (s.a.w.w.) mewaatangaza hao kuwa ni waghasibu wa ufalme.

kwa hakika warithi na makhalifa wa mtume (s.a.w.w.) ni maimam kumi na wawili ambao kama mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, ni katika kizazi bora cha Hashim wa kabila la Quraishi na kupewa madaraka juu ya viumbe vyote. walikuwa na elimu na uwezo wa kufanya (kuleta) miujiza(Karama) na sifa zote alikuwa nazo mtume (s.a.w.w.). kama alivyo yeye (mtume) walikuwa wametakasika kwa kila uovu na dhambi. hawa ni maimamu waliotajwa na allah katika qur'an tukufu kuwa ni "watu wa kweli wenye madaraka na walio takasika". mwanazuoni wa kisunni fak-ruddin razi, katika kitabu cha tafsir-al-kabir, juzuu la 3, ukurasa 357, chapa ya Misri, ameeleza kwamba amri ya "kumtii Mungu, Mtume wake na wale wenye madaraka" (4:54) inamaanisha kwamba wale wenye madaraka ambao utii wao uliamrishwa katika qur'ani ni wale tu wasio kuwa na dhambi na wasioweza kukosa; la sivyo, inamaanisha kwamba mungu ametuam risha kuwafuata wale wanaoweza kukosa kueleza amri za Mungu.
utambulisho wa hao maimam kumi na wawili warithi wa Mtume (s.a.w.w.), umethibitishwa na hadithi chache ambazo zimenakiliwa katika vitabu vya kisunni. Shaikhul islam, Sheikh Suleiman Hanafi Nehshabandi kanduzi Balkhi aliyefariki 1294 (a.h.) na aliyekuwa mtakatifu mkuu wa sultani wa istanbul (uturuki) Abdul aziz khan, ameandika katika kitabu cha yanabii -ul-mawaddah kurasa 369-71 (kama ilivyotafsiriwa katika kiingereza) "yahudi mmoja mwenye jina la naathal alikuja kuonana na Mtume (s.a.w.w.) na kutaka maelezo kuo.ndosha shaka alizokuwa nazo na kuahidi kwamba akipata maelezo ya kumtosheleza kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) atakubali dini ya uislam.
Mtume (s.a.w.w.) alimruhusu kuuliza maswali yake. kwanza yeye (naathal) aliuliza juu ya upwekee wa Allah na sifa zake, na kupata majibu ya kumtosheleza. baadaye akauliza maswali, juu ya urithi wa Mtume (s.avw.w.) na wa kila mtume na utangazaji wa warithi wao (warithi wa mitume kabla ya Muhammad (s.a.w.w.), kabla kufariki dunia k.m. nabii moosa alimteua yushae bin noon, Mtume (s.a.w.w.) akajibu "mrithi wangu mimi ni Ali ibn abi Talib, baada yake watakuwa wajukuu wangu wawili Hassan na Hussein na baada ya hao watakuwa maimam tisa ambao watatokana na kizazi cha Hussein (a.s.); nao ni warithi wangu". hapa huyo yahudi aliuliza majina ya hao maimam tisa na Mtukufu Mtume alisema "baada ya Hussein atakuwa mwanawe Ali ibni Hussein, na baada yake atakuwa mwanawe Muhammad bin Ali (Baqir)na baada yake Jaffer Sadiq na baada yake Mussa Kadhim na baada yake Ali Ridha na baada yake Muhammad Taki na baada yake Ali Naqi na baada yake Hassan na baada yake mwanawe Muhammad Mahdi.
hayo ndiyo majina ya warithi wangu kwa mpangilio huo". myahudi yule tena alimwomba Mtume (s.a.w.w.) amueleze hao warithi wake watatu yaani Ali, Hassan na Husein watafariki dunia namna gani. Mtume (s.a.w.w.) akamjibu "hadhrat Ali (a.s.) atauawa na upanga, Hassan atapewa Sumu na Hussein atauawa kwa (kuchinjwa) huku ana njaa na kiu ya siku tatu". myahudi tena akamwuliza Mtume (s.a.w.w.) kama hao mashahidi watakuwa na Mtume (s.a.w.w.) huko peponi. na hapo Mtume (s.a.w.w.) akajibu "hao watakuwa na mimi peponi". hapo myahudi akakiri shahada takatifu, na akawa mwislamu, na akasema "eh mtume wa mungu bila shaka hao uliowataja ni warithi wako. hao wametajwa kwa kirefu katika vitabu vya manabii waliopita na vilevile katika maagano ya nabii mussa. imeelezwa wazi humo kwamba atakuwa nabii katika kipindi cha mwisho akijulikana kwa majina ya Ahmad na Muhammad na ndiye wa mwisho wa manabii na baada yake hatakuwa nabii yeyote.
yeye (nabii) atakuwa na warithi kumi na wawili; wa kwanza ni binamu yake na mkwewe; wa pili na watatu watakuwa ndugu. mrithi wa kwanza atauawa kwa upanga, wa pili kwa sumu na watatu atauawa jangwani pamoja na wanawe na masahaba wake wakiwa na njaa na kiu ya siku tatu. watakabili misiba yote kwa subira na watapewa jazaa na mungu na kutukuzwa na uwezo wa kuokoa marafiki na wafuasi wake kutoka kwenda motoni. walio biki lisa watatokana na kizazi chake (Hussein) na kwa ujumla watakuwa kumi na wawili kama idadi ya "asbat". Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) baadaye akamwuliza kama anajua habari za asbat. yeye akajibu "ndiyo walikuwa kumi na wawili na katika hao lawa bin barkhya alighibu na kujitokeza tena na kupigana na mfalme wa karastya na kumwua". mtume mtukufu (s.a.w.w.) akaendelea kusema: "kwa hakika yale yaliyo wakabili mayahudi yatajiri kwa wafuasi wangu. mrithi wangu wa kumi na mbili ataghibu. katika siku hizo uislam utabakia kwa jina tu. qur'an itasomwa kama kawaida ya dini lakini bila kufuatwa kwa vitendo.
wakati dhulma (kufuru) itakapokuwa imetawala mrithi wangu wa kumi na mbili atajitokeza na kuufufua tena uislam, haki na insafu. watao bahatika ni wafuasi wale ambao wataomtii yeye (Mahdi) na ghadhabu ya Mungu itawasubiri wale ambao watamhalifu yeye (Mahdi)." tena katika kitabu hicho, ukurasa 371, sura ya 77, kuhusu hadithi ya mrithi wa kumi na mbili ameeleza chini ya kichwa cha 'tahkik' (uthibitisho) kuwa: "imesimuliwa kwamba jabir bin saamra, mmojawapo wa masahaba wa mtume (s.a.w.w.), amesema kwamba uislam utadumu kwa sababu mrithi wangu wa kumi na mbili atakuwepo na warithi wangu wote watatokana na nambari ya qureish." vitabu vilivyo andikwa na bukhari, muslim na tirmidhi vinaeleza hadithi hiyo ilivyo. zaidi ya hayo yahya bin hassan katika kitabu chake umdah ameelezea kwamba kuna hadithi 20 za Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) za kusimulia kwamba warithi wake kumi na wawili wote watatokana na mbari ya quraish.
vitabu mashuhuri vya sunni kama vile vya bukhari na Hamid vimesimulia hadithi tatu na. Tirmidhi vile vile kaandika hadithi moja juu ya jambo hilo. Muslim aandika kwamba Abdi Saad, Sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) alimwandikia samra kumwuliza kwamba alisikia hadithi yoyote kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Samra katika jibu akaeleza kwamba siku ya ijumaa ambayo Aslami alipigwa mawe mpaka akafariki, Mtume (s.a.w.w.) alisema uislam utaendelea mpaka siku ya kiyama na watakuwa warithi wake kumi na wawili baada yake na wote watatokana na ukoo wa quraishi. hadithi nyingi zilizoandikwa katika vitabu vya sunni zathibitisha kuwapo kwa warithi kumi na wawili waliotajwa na Mtume (s.a.w.w.) wanatokana na ukoo wa Quraishi. kwa hakika warithi kumi na wawili waliotajwa hawawezi kuwa wengine ila wale tu wanaokubaliwa na mashia ithnaasheri. hawawezi kuwa na uhusiano wowote na makhalifa wa bani umayya kwa sababu hawakuwa kumi na wawili na ambao walikuwa wadhalimu ila mmoja Omar bin Abdulaziz ambaye alikuwa mwema. vile vile hao bani umayya hawakuwa katika kizazi cha Hashim kama ilivyoelezwa katika hadithi nyingi za Mtume (s.a.w.w.). vile vile hawawezi kuwa makhalifa wa bani abbas kwa sababu hawakuwa kumi na wawili na walikuwa madhalimu na maadui wa Ahlul Bait wa Mtume (s.a.w.w.).
hivyo, uhakika ni kuwa warithi kumi na wawili waliotangazwa (tajwa) na Mtume (s.a.w.w.) ni maimam kumi na wawili kutokana na dhuria ya mtume (s.a.w.w.) na katika uhai wao hawakuwa na mtu yeyote aliyelingana nao katika elimu, ibada, atakuwa na ushujaa. hakuna wengine wanaostahili sifa zilizoelezwa kutokana na hadithi za Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa hao maimam kumi na wawili. tena katika kitabu hicho hicho sura ya 78, ukurasa 374, mwandishi amenakili: "katika kitabu faraedussimtayn imeelezwa kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) ameeleza bayana kwamba yeyote asiye amini katika kujitokeza kwa mehdi ni kafiri na yeyote asiye amini kuja kwa nabii issa kutoka mbinguni vile vile ni kafiri na yeyote asiye amini kujitokeza kwa dajjal mwenye jicho moja tu vile vile ni kafiri."
zaidi ya hayo, katika kitabu hicho hicho imesimuliwa hadithi kutoka kwa mtume mtukufu (s.a.w.w.) iliyo andikwa na ibnu abbas kwamba yeye (mtume) amesema "watakuwa warithi kumi na wawili baada yangu ambao watakuwa Hujjah (dalili) ya Mungu juu ya viumbe wake. wa kwanza atakuwa hadhrat Ali (a.s.) na wa mwisho hadhrat Mahdi (as.). wakati huo wa mehdi (a.s.) ardhi itang'aa na utawala wake utaenea kote kote duniani".
waislamu wote, mashia na masunni, huamini kwamba watakuwa warithi kumi na wawili wa Mtume (s.a.w.w.). hivyo imebainika kutokana na hadithi mashuhuri kwamba warithi wa kweli kumi na wawili kufuatana na hadithi za Mtume (s.a.w.w.) ni wale kumi na wawili wanao kubaliwa na shia ithnaasheri; wa kwanza ni Ali ibn abi Talib (a.s.) na wa mwisho wao ni imam wa kumi na mbili imam hadhrat Muhammad Mahdi (a.s.). hata hivyo, kuna hadithi mbili katika vitabu vya sunni zinazonakili majina ya maimam kumi na wawili. itabainika kuwa kukamilisha idadi hiyo ya kumi na wawili, hadithi hizo zinamtaja muawiyya pamoja na mwanawe yazid n.k. ambao hawastahili kuitwa warithi wa Mtume (s.a.w.w.). Mulla Alikari katika kitabu cha 'Sharhe Mishkat' na tena katika kitabu 'Sharhe Akhbar' amenakili majina kumi na mbili y amakhalifa wanao aminiwa na masunni. 1) Abu Bakar 2) Omar 3) Uthman 4) Hadhrat Ali (a.s.) 5) Muawiyya 6) mwana wa Muawiya Yazid 7) Abdul Malik bin marwan na wanawe wane 8) Walid 9)Suleiman 10)Hisham 11)Yazid 12) Omar bin Abdulaziz. Suyuti katika kitabu 'Tarikhul Khulafaa' (historia ya makhalifa) amenakili kutoka sahihi Bukhari na Sheikhul islam ibnu hajar kuwa: "kutokana na hadithi zinazo kubalika, waislamu wanakubaliana kuwepo makhalifa wafuatao:
1) Abubakar 2) Omar 3) Uthman 4) Hadhrat Ali (a.s.) na baadaye hapakuwa na makubaliano juu ya urithi wa imam Hassan (a.s.) kulikuwa na mapatano ya kumkubali 5) muawiya na baadaye imam Hussein (a.s.) ambaye hakurithi kwa sababu aliuawa "shaheed", kwa hivyo 6) Yazid alikubaliwa na watu wakala kiapo cha utii kumkubali yeye yazid. baada ya kifo cha yazid kulikuwa na mafarakano juu ya urithi lakini wengi wakamkubali abdul malik baada ya kuuawa ibnu zubeir. (baada ya yazir marwan alitawala kwa muda ya miezi sita tu na mwanawe abdul malik aliendelea kwa miaka 21 lakini wote wawili hao hawakuorodheshwa). katika orodha ya makhalifa kutoka taarifa tuliyotaja kwanza abdul malik ametajwa ni khalifa wa saba lakini katika orodha ya pili ya makhalifa hakutajwa kabisa.
baada ya yazid wana wanne wa abdul malik wanakubaliwa kuwa warithi, nao ni 7) walid 8) Suleiman 9) Yazid 10) hashim na baada ya hao 11) Omar bin abdulaziz (kama alivyoorodheshwa wa kumi na mbili katika orodha ya kwanza kutokana na hadithi) 12) walid ibnu yazid ibnu abdul malik bin marwan (ambaye kutokana na hadithi iliyotajwa atakuwa khalifa wa kumi na tatu). kwavyo, huthibitika kutokana na maandishi ya waislamu mashuhuri na hadithi za kuaminika kwamba maimam kumi na wawili wanaofuatwa na shia ithnaasheri ni warithi wa kweli. katika hao wa kwanza ni hadhrat aii ibn abi talib (a.s.) na wa mwisho ni Hadhrat Mahdi (a.s.)..
http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&Id=264524

Comments