TAREHE YA KUZALIWA MTUME (s.a.w.w)

TAREHE YA KUZALIWA MTUME (s.a.w.w)
Katika kitabu cha historia cha Qadhi Husain Ibn Muhammad Diyar
Bakari al-Maliki inayoitwa Tareekh-e-Khamees, imeandikwa hivi kwamba Mtume wetu alizaliwa mwezi kumi (10) Rabi-ul-Awwal,
na kwa mujibu wa walivyopokea wengine, tarehe ya kuzaliwa kwake ni kumi na mbili (12) Rabi-ul-Awwal na wengine wamepokea kuwa ilikuwa kumi na saba (17) Rabi-ul-Awwal. Kwa nchi za kiislamu kama Iran wiki nzima ya kuanzia 12 mpaka 17 huwa ni wiki ya sherehe ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w) ili waislamu wa madhehebu yote washiriki katika ibada hii muhimu ya kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi wa Ummah huu. Wiki hii huitwa wiki ya umoja na watu hawaende kazini kwa wiki nzima.


Suala la mwaka halina ubishi kwani wote wameandika kuwa kwa kalenda ya waarabu kipindi hicho, mwaka aliozaliwa Mtume (s.a.w.w) ulikuwa ukiitwa mwaka wa tembo (A’mul fiil). Isipokuwa waandishi wamekhitilafiana tena kuwa mwaka huo unalingana na mwaka gani ya miladia au Gregorian callender. Wapo waliosema ni mwaka wa 570 AD na wengine walisema kuwa ni mwaka 571 AD. 

Comments