Amesema
Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kuna muumba asiyekuwa Mwenyezi
Mungu" Qur'an, 35:3
Na Amesema
tena:
"Waambie,
Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu" Qur'an, 13:16.
Umma
umekubaliana juu ya Tauhidi yake katika Rububiya yake na kwamba hapana Mola
wala mwenye kusimamia (mambo yao) asiyekuwa yeye.
Amesema
Mwenyezi Mungu:
Yeye ndiye
anayesimamia mambo yote hakuna muombezi ila baada ya idhini yake, huyo ndiye
Mwenyezi Mungu Mola wenu basi muabuduni yeye, Je, hamna kumbukumbu?
Pia
wamekubaliana kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada na kwamba, yeye Mwenyezi
Mungu ndiye Mola ambaye anastahiki kuabudiwa na hakuna wa kuabudiwa asiyekuwa
Yeye.
Mwenyezi Mungu
Amesema:
"Waambie,
Enyi mliopewa Kitabu, njooni kwenye neno lililo sawa kati yetu na ninyi ya
kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, na wala tusimshirikishe na
chochote, wala baadhi yeta tusiwafanye kuwa waungu badala ya Mwenyezi
Mungu". Qur
'an, 3:64
Bali hizi ndizo
nukta ambazo zenye kuafikiana baina ya sheria za mbinguni. Basi mtazamo ulio kinyume
na misingi hii ni miongoni mwa vitendo vya uchafuzi na kupotoshaji.
Na wapotoshaji
hao si wengine bali Mawahhabi ambao wanajifanya kuwa wanajifanya kuwa wanafuata
tawhiid halafu wanapotosha dhati ya Mwenyezi Mungu ili waweze kuwakufurisha
waislamu wa kisawasawa ambao ni Mashia na ndugu zao AhlulSunnah waljamaa.
Comments
Post a Comment