TAWHEED KWA MUJIBU YA SHI’A ITHNA’ASHARA

Kuna Mungu Mmoja tu (Allah), wa milele, hana mwanzo wala mwisho, ni mwenye kujitosheleza. Mungu mwenye enzi na nguvu na anauwezo juu ya kila kitu na kila jambo, ni mwenye kujua yote, hakuna kilicho siri kwake.
Allah (S.A.W) ana hiari juu ya mambo yote, halazimishwi, ni mwenye kutambua, na ni mwenye kuona kila kitu, ni mwenye kusikia kila sauti, yuko kila mahali, Yeye anaona kila kitu ingawa hana jicho wala sikio.
Mwenyezi Mungu hana mshirika wala mwenzi, wala hana mtoto yeyote wala mke. Hakutengenezwa wala hakubuniwa kwa kitu chochote cha maada. Hana mwili wala sehemu mahala pa kuwepo, hadhuriwi na kitu chochote kinachohusiana na mwili. Haongozwi na wakati mabadiliko au vitu kama hivyo.
Allah haonekani, hajaonekana, na wala hataonekana si hapa Duniani wala Akhera. Sifa zake hazikutengwa na dhati yake. Husema kweli na ni Mkweli. Haingii kwenye mwili wowote, Hahitaji kitu chochote, na hafanyi ubaya. Ni yeye aliyeumba mbingu na Ardhi na ni Yeye Mwenye kuzihifadhi na kuziruzuku.
Soma kitabu kinachoitwa “Maana na Asili ya Ushia,” cha Allamah Akhatar Rizvi aliyekuwa mubaligh mkuu wa Tanzania

Comments