TAWHID KWA MUJIBU WA MASALAF, ANSWAR SUNNAH.

Imani hii potofu inatokana na fikia ya Sheikh mpotofu aitwaye Ibn Taimiyyah ambaye ametuarifisha maana ya Tauhidi katika kitabu chake aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu ya mbingu yake kwenye arshi yake, yuko juu ya viumbe wake"
Na amesema tena: "Mola wetu hushuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila siku inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku kisha husema; Nani ataniomba (saa hizi) nami nitamkubalia (maombi yake), nani ataniomba nami nitampa, ni nani atanitaka msamaha nami nitamsamehe".
Haya ndiyo maarifa ya sheikh huyu ambayo wao humwita sheikhul Islam (Ibn Taimiyyah) na huku ndiko kumtakasa kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na (yote haya aliyoyasema) inajulisha wazi kabisa kuwa yeye anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anao mwili na anapatikana upande fulani. Na (huyu Ibn Taimiyyah) amesema hayo kutokana na kung'ang'ania kwake dhahiri ya aya na hadithi za Mtume bila ya kuzitafiti kwa undani aya zilizokuja kuhusu maudhui hiyo, na bila ya kufanya uhakiki katika isnadi za hadithi na madhumuni yake.
Imani hii potofu ilirithiwa na masheikh wengine wa kisalafiya na Answar Sunnah kama Ibn Al-Qayyim na Muhammad bin Abdul-Wahhab. Na cha ajabu ni kwamba, hawa nao wanataka wawe ni waalimu wa Tauhidi na walinganiaji wa Tauhid.
Rejea:
Maj-mu'a 'Tur-Rasailil-Kubra, cha Ibn Taimiyyah, Al-A'qidatul-Wasitiyah uk. 401.

Watu hawa kwa sababu ya kung’ang’ania kutafsiri aya za Qur’an na hadith za Mtume bila ya kusoma Uislamu kwa undani wake wamekuwa wakichagua aya zinazohimiza vita na kuzitafsiri vibaya kama ushahidi wa kuwauwa na kuwadhalilisha wanadamu, na kuzitupilia mbali aya nyingi tu za Qur’an ambazo zinahimiza upendo, amani na umoja. Vile vile Qur’an tukufu inahimiza watu wawe wasamehevu lakini wao wanafundisha wafuasi wao wawe wababe na wajeuri.

Comments