UFAFANUZI WA AYA YA QUR'AN (98:7)
Ibn Asakir anasimulia kutoka kwa Jabir bin Abdallah ambaye alisema, 'Tulikuwa pamoja na Mtume wakati Ali (a.s) alipokuja, Mtume akasema, “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hakika huyu Ali na Shi'a wake ndio wenye kufuzu siku ya ufufuo,” kisha aya ifuatayo ikashuka, “Hakika wale walioamini na kutenda mema, basi hao ndio wema wa viumbe”' (Qur'an 98.7). Kwa maalezo yaliyotangulia inaonesha wema wa viumbe ni Imam Ally (a.s) na Mashia wake.

Tazama kitabu kiitwacho Ad-Durrul Manthur cha As-Suyut J.6 uk 379, na Al-Manakib cha Khwarizini.
At-Tabarani anasema kwamba, Mtume alimwambia Ali, “Ewe, Ali, hakika wewe utakuja mbele ya Allah ukiwa na Mashia wako hali ya kuwa mmeridhika (na Allah) na hali ya kuwa mmeridhiwa na Allah”.
Soma As-Sawaiq'l Muhriqah cha Ibn Hajar al-Makki (chapa ya Cairo) uk. 92. Anasimulia hadith nyingi zenye maana kama ilivyo hapo juu
Comments
Post a Comment