Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo mna madhara makubwa na (baadhi ya) manufaa kwa (baadhi ya) watu. Lakini madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.” (Al-Baqarah: 219)
Vile vile twaambiwa katika Ayah nyingine:
“Kwa hakika Shaitani anataka kukutilieni uadui na bughudha baina yenu kwa kutumia ulevi na kamari na anataka kukuzuilieni dhikri za Allah na kusali. Basi je mtaacha hayo? (Al - Maida: 93)
Kuna watu wanawadanganya wengine ili waamini kuwa iwapo pombe ikinywewa kwa kiasi kidogo, basi haitakuwa na madhara bali kutakuwa na faida ndani mwake. Lakini kutokana na utafiti uliofanywa na Wanasayansi wa Marekani na Ulaya imebainika wazi wazi kuwa pombe kwa kiasi kidogo kabisa pia kinaleta madhara makubwa kwa mnywaji.
Tafadhali zingatia ripoti ifuatayo ambayo imepatikana:
Wakati fulani ambapo mabingwa wa fani ya utabibu walipokusanyika katika kongamano lao la kimataifa huko Washington, Marekani kwa ajili ya kupiga vita pombe na unywaji wake, nao walitoa kauli moja kuwa pombe ndiye adui no. 1 wa mwanadamu.
Dr. Melvin Kanzeli, ambaye amepitisha miaka mingi katika utafiti juu ya unywaji wa pombe, alisema yafuatayo katika kikao hicho kuwa:
“Unywaji wa pombe unaharibu sana ubongo wa mtu. Wakati mtu ajisikiapo raha na kuburudika kwa kiwango kidogo cha pombe, yeye huwa hana habari kuwa anaziua seli za ubongo wake.”
Dr. Kanzeli ambaye ndiye Mkuu wa taasisi ya utafiti cha Chuo cha Matibabu cha South Carolina, anaamini kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi unasababisha mabadiliko katika damu na mishipa yake kiasi kwamba ubongo unakosa hewa ya oksijeni na hivyo kuharibiwa, au kuharibika kiasi kwamba mtu anatumbukia katika hali ya kuchanganyikiwa akili.
Kuingia kwa pombe katika damu kunaathiri mno mzunguko wa damu, na hivyo mara nyingi husababisha kuganda kwa damu.
Dr. Raymond Penington, naye pia katika ripoti yake ya kurasa 4 aliyoiwasilisha katika kongamano hilo, alisema:
“Hakuna shaka kuwa pombe ndiye adui hatari mkubwa sana wa mwanadamu, na wale wote wanaojitamba kuwa wao wanakunywa kwa nadra sana, nao pia wanajitumbukiza katika matokeo maovu kabisa ya adui huyu.
Katika maoni yake, matokeo ya awali ya unywaji wa pombe ni usahaulivu na hatimaye kupoteza kazi aliyokuwa akiifanya mtu. Yeye anasema:
Utafiti wetu umetuonyesha kuwa walevi katika muda mfupi huanza kusahau - sahau na hivyo hujikosesha nafasi ya kujipatia maendeleo. Wao huwa hawana hamu na kazi zao, na hatimaye kupoteza kazi zao jambo ambalo litatumbukiza zaidi katika pombe.”
Hivyo nakuombeni kwa wale ambao hatujawahi kunywa tuendelee na msimamo huo na wale wanakunywa waache.

Comments
Post a Comment