UIMAMU (UKHALIFA)
Msimamo wa
Aya zilizokuja juu ya uongozi ukisoma yalioandikwa katika vitabu mbali mbali na
Hadithi zilizothibiti, na tarikh inayoonyesha katika jambo hili, utapata mambo
makuu matatu ambayo yanaonyesha kuwa:
Uimamu/Ukhalifa
lazima uteuliwe na Mwenyezi Mungu. Na kwa upande wa pili utaona kuwa Nyimati
zilizopita zilifuata uongozi uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu, wala jambo hilo
halikuachiwa watu wenyewe kwa njia ya kuchaguwana.
Jambo la
kwanza lililoongoza baina ya Mitume waliopita ilikuwa ni kusalimu amri na
kufuata uongozi wa Mwenyezi Mungu, na kila alipoondoka Mtume aliweka
atakaeshika nafasi yake. Wengi wao waliorithi kazi zao walikuwa Manabii, hata
hivyo baadhi yao hawakuwa Manabii bali walikuwa Mawasii tu.
Jambo la
pili: Uongozi katika nyimati zilizopita ulipatikana kwa njia ya kurithi baina
ya vizazi katika koo za Mitume kama tunavyosoma katika Aya zifuatazo: a.
"Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na Kizazi cha Ibrahim na
Kizazi cha Imrani juu ya walimwengu wote. Ni kizazi cha wao kwa wao, na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua" 3:33-34
b. "Na
tulimpa Isihaqa na Yaaquubu na tukaweka katika Kizazi chake Unabii na Kitabu,
na tukampa ujira wake katika dunia. Nae katika akhera kwa hakika atakuwa
miongoni mwa watu wema." 29:27
c. "Na
hakika tulimpeleka Nuhu na Ibrahim na tukauweka katika kizazi chao Unabii na
kitabu." 57:26
d. Mwenyezi Mungu alimweka Ibrahim kuwa Imam (Kiongozi wa watu). Ibrahim alimuomba Mola wake awape nafasi hiyo vile vile katika kizazi chake. Mwenyezi Mungu hakumkemea wala kumgombeza, ila alimwambia ya kuwa: "Haiwafakii ahadi yangu (Unabii and Uimam) watu madhalimu." 2:124.
d. Mwenyezi Mungu alimweka Ibrahim kuwa Imam (Kiongozi wa watu). Ibrahim alimuomba Mola wake awape nafasi hiyo vile vile katika kizazi chake. Mwenyezi Mungu hakumkemea wala kumgombeza, ila alimwambia ya kuwa: "Haiwafakii ahadi yangu (Unabii and Uimam) watu madhalimu." 2:124.
e. Nabii
Musa (a.s.) alipoomba kwa Mwenyezi Mungu ndugu yake Haruna awe msaidizi wake
katika uongozi, Mwenyezi Mungu hakumkasirikia wala kumkatalia ombi hilo.
"Na unijaalie waziri katika jamaa zangu, Haruna ndugu yangu. Uniimarishe
kwake nguvu zangu, na umshirikishe katika kazi yangu. Ili tukutukuze sana, na
tukutaje kwa wingi. Hakika wewe unatuona, akasema hakika umepewa maombi yako
ewe Musa" 20:29-36.
Musa
alimweka Haruna kuwa Khalifa wake alipoondoka, kama Quran inavyosema: "Na
tulimwahidi Musa siku thelathini na tukatimiza kwa kumi ikatimia miadi ya Mola
wake siku arobaini. Na Musa akamwambia ndugu yake Haruna: Shika mahala pangu
katika watu wangu na usuluhishe wala usifuate njia ya waharibifu." 7:142
Katika Aya hizi tumeona nafasi ya Uongozi inavyoendelea kati ya Kizazi na Kizazi
baina ya koo za Manabii.
Utaratibu ni
huu wa mtume kuweka mrithi wake katika uongozi, na ndivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w)
alimteua imam Ally (a.s) kuongoza umma wakati atakapofariki dunia. Lakini wababe
wakapinga na kuchukua madaraka kwa nguvu. Na huo ndio mwanzo wa mgawanyiko kwa
waislamu. Waliafikiana na Mtume juu ya ukhalifa kuwa wa Imam Ally huitwa Mashia
na wale waliopinga na kuamua kuchaguana na ndipo Abubakar alipochaguliwa hutwa
Ahlulsunnah waljamaa.
Comments
Post a Comment