Madhehebu ya Jaafariyyah (Shia Ithnaashara) ndio Uislamu halisi kutokana na misingi yake kutoka kwa Mtume wa Uislamu, yaani Mtume Mohammad Mustafa (S.A.W.W). Fiq-hi ya kwanza ndani ya Ulimwengu wa kiislamu iliandikwa na Imam Jaafar Swadiq (a.s), kutokana na fiq-hi hii ndipo Madhehebu mengine yakachakachua na kupata Fiq-hi zao ambazo zinaitwa Fiq-hi za madhehebu manne yaani Hanafi, Shafi, Maliki na Hambali. Fiq-hi hizi nne ndio zinazofuatwa na Masunni. Cha kushangaza Sunni ambao ni watoto wa Shia, wanajifanya kuwa wao pekee ndio waislamu na kufanya uadui na mauaji dhidi ya Mashia. Ninawaomba wasome Historia za waanzilishi wa Madhehebu zao na watambue walimu wao. Watagundua kuwa Maimamu hao wa Sunni wamefundishwa na Maimamu wa Shia.
Kwa mfano Imam Abu Hanifa amesoma kwa Imam Jaafar Swadiq (a.s), na kwa hili Abu Hanifa anasema, “Lau kama si miaka miwili niliyosoma kwa Imam Jaafar Swadiq, basi Nuuman angeangamia.”
Usomaji wao ulikuwa hivi: Imam Ahmad bin Hambali amesoma kwa Imam Shafii, Shafii naye alisoma kwa Maliki, na Maliki alisoma kwa Abu Hanifa, na Abu Hanifa alisoma kwa Imam wa sita wa Shia (Imam Jaafar Swadiq ambaye ni Jaafar bin Mohammad). Huyo ndiye mtu wa kwanza kufungua chuo kikuu cha kiislamu ndani ya msikiti wa babu yake yaani Mtume Mohammad (S.A.W.W).

Comments
Post a Comment