UJUMBE WA UISLAMU

Shukurani zote zinamsitahiki Mwenyezi Mungu,na rehma na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na maswahaba zake waliokuwa wema.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Sema; Enyi watu mlio pewa kitabu (cha Mwenyezi Mungu. Mayahudi na Wakristo)! njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu; ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu,wala tusimshirikishe (Mwenyezi Mungu) na chochote,wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu (au pamoja na Mwenyezi Mungu). wakikengeuka, semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni waislamu, (tumenyenyekea amri za Mwenyezi Mungu”).1
1 Al imran: 64
2 Al aaraf :33
Kwa hakika dini ya Uislamu ndiyo dini ya haki, kwa kuwa ndio dini ya kimaumbile iliyo sahihi, dini iliyo wazi ambayo hakuna ndani yake ugumu wowote wala uficho wa aina yeyote, kila mtu katika Uislamu ana haki ya kuuliza chochote kinacho mtatiza, au jambo lolote linalo msumbua katika akili yake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “ Sema (uwaambie): “Mola wangu ameharamisha mambo machafu, yaliyodhihirika na yaliyo fichika, na dhambi na kutoka katika utii (wa wakubwa) pasipo haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika ambacho hakukiteremshia dalili (ya kusema kishirikishwe naye) na (ameharamisha)kusema juu ya Mwenyezi mungu msiyo yajua”.2
Bali Uislamu umetoa haki ya kujibu mambo yanayo fungamana na dini kwa watu wenye elimu ya kisheria, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: “… Basi waulizeni wenye kumbukumbu (za vitabu vya Mwenyezi Mungu vya kale) ikiwa nyinyi hamjui’3
3 Annahli :43
Anayeulizwa ni bora awe mjuzi kweli kweli kwa sababu kama ukipata maarifa kwa mtu asiye na ujuzi sahihi wa Uislamu basi atakupotosha na utajikuta unakuwa mwislamu wa ajabu ajabu kama vile takfir.

Tunamwomba Allah atuepushe kuwafuata watu wajinga na pia atuepushe kuwa katika makundi ya watu wanaofuata maslahi ya kidunia na kuisahau akhera huku wakiitaka. 

Comments