Kwa upande wa Madhehebu ya Shia
Ithnaashara: Mojawapo ya madhambi ambayo yamechambuliwa kama ni miongoni mwa
dhambi kuu ni ulawiti au kuingiliana jinsia moja. Hivyo imethibitishwa na
al-Imam as- Sadiq (a.s.) na Al-Imam Ali ar-Ridha (a.s.). Kwa hakika dhambi hili
ni kubwa hata kuzidi dhambi ya zinaa. Madhambi na adhabu yake ni zaidi ya zinaa.
Amesema al-Imam as- Sadiq (a.s.) katika Al-Kafi :
“Kuingiza uchi wako mwanzoni mwa sehemu ya
nyuma ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika uke. Kwa hakika Allah
(swt) ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut (a.s.) kwa sababu wao walijiingiza
katika laana ya ulawiti. Allah (swt) kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa
dhambi ya zinaa.”
Amesema Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika
Wasa’il al-Shiah :
“Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na
kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata
kwa maji ya dunia nzima. Allah (swt) atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani
Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Moto yaani
Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa! Pepo (Jannah) zitakuwa
zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah (swt)
humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko
hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha
kuwekwa Motoni rasmi. Atapitia adhabu moja baada ya yapili hadi kuzimaliza
adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe
hataweza kutoka hapo.”
Comments
Post a Comment