UMAR BIN KHATAB, KHALIFA WA PILI KUPITIA WAPINZANI WA MTUME (S.A.W.W)

UMAR BIN KHATAB, KHALIFA WA PILI KUPITIA WAPINZANI WA MTUME (S.A.W.W)
Kipindi kabla ya Uislamu Umar alikuwa dalili na kabla ya hapo alikuwa mchungaji wa ngamia. Kipindi hiki Umar alikuwa adui mkubwa wa Mtume na waislamu kwa ujumla. Yeye aliukubali Uislamu baada ya miaka sita tokea Mtume (s.a.w.w) atangaze utume wake.
Baadhi ya wanahistoria wanadai kuwa Umar bin Khatab alikuwa shujaa kiasi kwamba kuingia kwake katika Uislamu kuliwatia hofu kweli kweli waabudu masanamu. Lakini ukweli unaonesha kinyume cha hayo. Kwani wakati Umar alipoukubali Uislamu makafiri walibaki na ukafiri wao na hakuna chochote kilichobadilika. Badala ya kupata ahueni tulishuhudia Mtume wetu akilazimika kuikimbia nyumba yake kwa miaka mitatu akaishi katika pango kwa amri ya Maquraish, kipindi hiki alikumbana na njaa kali sana na mazingira yanayohatarisha maisha yake. Kipindi hiki Umar na Abubakar walikuwa Makah wakila kuku kwa mrija na hawakuchukua hatua yoyote iwe ni kuzuia tatizo hili au kumsaidia Mtume na familia yake waliokuwa wanateseka kwa njaa.
Miaka michache baadaye Mtume alilazimika kuikimbia Makah na kwenda kwanza Taif ambako alikumbana na madhila makubwa kuliko hata ya Makah na kisha baadaye alihamia kwenda Madina. Kabla ya kuondoka Maka makafiri walikuwa wameizunguka nyumba ya Mtume tayari kwa kumuua. Je Umar na ushujaa wake alifanya nini ili kumnusuru Mtume katika hali hii ngumu?
Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufika Madina na Masahaba kumfuata, alitengeneza undugu baina ya masahaba ili waweze kusaidia kutokana na kwamba Muhajirina walikuwa wameacha familia zao Makah hivyo wanahitaji familia. Katika tukio hili Mtume alimpanga Imam Ally kuwa ndugu yake na Umar akapangwa kuwa ndugu wa Utban bin Malik.
Katika mwaka wa tatu bint wa Umar aitwaye Hafsa aliolewa na Mtume
Umar bin Khatab alikimbia Jihad mara kadhaa. Mojawapo ni vita Uhudi kiasi kwamba Yeye mwenye Umar anasema kuwa nilikimbilia mlimani (Suyuti katika Al-Durrul Al-Manthur). Katika vita vya Khaibar Umar aliongoza jeshi lakini akashindwa kuleta ushindi. Katika vita vya Hunain alikimbia vita kiasi kwamba Abu Qatada mmoja wa Masahaba wa Mtume anasema kuwa katika vita ya Hunain wakati waislamu walipokimbia vita, nami nilikimbia na nikamwona Umar na wengine wengi wakikimbia (Bukharin a Kitabul Maghazi).
Katika mwaka wa nane Hijriya Umar alitumwa na Mtume katika vita iitwayo Dhat es Salasil, chini ya uongozi wa Amr bin Aas kama kamanda.
Mwaka wa 11 Hijriya, Mtume aliandaa jeshi kwenda Syria na akamteua Usama bin Zaid bin Hatith kama kamanda. Mtume alimwamuru Umar ajiunge na jeshi la Usama.
Pamoja na kwamba Umar aliishi na Mtume kwa miaka 18 akiwa sahaba wake, hakuweza kupewa cheo chochote na Mtume kiwe cha kiraia au kijeshi isipokuwa kimoja tu kile cha kuongoza vita vya Khaibar ambapo alishindwa vibaya sana na kukimbia. Ushindi ulipatikana kesho yaka chini ya uongozi wa Imam Ally (a.s).

Tutaendelea na Historia hii ya Khalifa Umar bin Khatab Inshallah. 

Comments