UMUHIMU WA SWALA
“ewe Mola wangu
Mlezi! nijaalie niwe msimamishaji Swala na kizazi changu, Mola wetu! na upokee
maombi yangu”1
Anasema Imam Al- Baqir (a.s): “Kitu cha kwanza
atakachohesabiwa muumini (Siku ya Kiyama) ni Swala, ikikubaliwa yatakubaliwa
matendo mengine, na ikikataliwa basi yatakataliwa matendo mengine.”2
Nadhani unafahamu kuwa kama matendo yako yote yakikataliwa na Allah (s.w.)
itakuwa na maana kuwa wewe ni mtu wa jahanamu.
Rejea:
1. Sura Ibrahim: 40.
2. Biharul-An'war, Juz. 47 Uk. 2.
Hivyo basi hakuna mjadala, endapo kama unataka kuokoka
kutokana na adhabu ya Allah (s.w) huna budi uanze kuswali leo. Usingoje maana
hujui utakufa lini? Kwa bahati nzuri huu ni mwezi wa Ramadhani ambao ni mwezi
wa toba, akianza ibada ndani ya mwezi huu na ukatubia na kuazimia kuwa
hutorejea kufanya maovu tena,basi Allah (s.w) atakusamehe, insha-Allah.
Comments
Post a Comment