Allah (s.w) anasema Qur’an tukufu (2:124)
kuwa, Na (kumbukeni) Ibrahim alipojaribiwa na Mola wake kwa matamko, na
akayatimiza. Akasema: Hakika mimi nitakufanya imam wa watu (Ibrahim) akasema:
Je, na katika kizazi change (pia). Akasema (ndiyo, lakini) ahadi yangu
haiwafikii madhalimu.
Hapa pana mambo matatu ya kuchunguzwa: (a)
Matamko aliyojaribiwa Ibrahim na Mola wake (b) Mimi nitakufanya Imam wa watu
(c) Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.
a) Matamko aliyojaribiwa Ibrahim: Aliulizwa
Imam Ja'afar As'sadiq (a.s) kuhusu Aya hii, akajibu: Ni yale yale maneno
aliyoyasema Nabii Adam (a.s.) kumuomba Mola wake: Ee Mola! Ninakuomba kwa haki ya Muhammad
na Ali na F'atima na Hasan na Husein (a.s.). Akaulizwa tena Imam Ja'afar
As'sadiq (a.s) maana ya 'FA ATAMMA HUNNA" yaani: "Na
akayatimiza" Akajibu: "Ameyatimiza kwa Imamul qaaim, Imam wa kumi na
mbili katika Ahlul Bayt aliotuachia Mtume (s.a.w.)
Tazama:
Al'bur'han fyi tafsiril
Qur'an J.l Uk. 147
Majmaul Bayani J.l
Uk. 378
Tafsirus Saafy
J.l Uk. 186
b) Mimi nitakufanya Imam wa watu: Ahadi ya
Mwenyeezi Mungu, ambayo ndiyo Uimam anaopewa Ibrahim, ni: ''Al-Imamah''.
Taz: Tafsirul
Qurtubi J.2 Uk. 108
Zaadul masir J.l Uk. 140
c) Ahadi yangu haiwafikii madhalimu.
Kiongozi atakaeshika nafasi baada ya Mtume ni lazima awe safi, kama Mwenyeezi
Mungu anavyowasifu: "Na jueni ya kwamba Mtume wa Mwenyeezi Mungu yuko
pamoja nanyi, lau yeye angewatiini katika mambo mengi lazima mngetaabika.
Lakini Mwenyeezi Mungu ameipendezesha kwenu imani, na amezipamba nyoyo zenu, na
amekufanyeni mchukie ukafiri na ufasiqi na uasi, hao ndio waliongoka"
49:7.
Msimamo ulioonyeshwa hivi karibuni na baadhi
ya Waislamu wa Tanzania kuhusu haja ya kuwa na kiongozi muadilifu, ni ishara
muafaka na qadhia hii.
Comments
Post a Comment