USHAHIDI
WA IMAM ALLY (A.S) KUDHULUMIWA UKHALIFA
Kuna watu
wananihoji kama ninaushahidi wa kuthibitisha kuwa Imam Ally (a.s) alidhulumiwa
ukhalifa na Abubakar bin Quhafa. Nimetafuta katika vitabu na hatimaye nimeupa
ushahidi mzuri sana. Kwa sababu msemaji ni yeye Mwenye Abubakar na pili kitabu
nilichokirejea ni cha Kisunni. Baada ya hili ninawaombeni wote sasa mmuunge
mkono Imam Ally (a.s) na Ahlulbayt wa Mtume (s.a.w.w) kwa ujumla.
Ibn Abil
Hadid Mu'tazil katika Sharh-e-Nahajul Balagha jz 4 uk 80 ameandika kuwa Abubakar
swidiq alimtukana Ally bin Abu Twalib na bibi Fatwima (a.s) kama ifuatavyo
"enyi watu! Kwa nini mnachanganyikiwa hivi? Kwa nini mumsikilize kila mtu?
Kwa vile tu nimekataa ushahidi wao wanazungumza upumbavu. Ukweli ni kwamba yeye
ni mbweha ambaye amesalitiwa na mkia wake... Yeye ni sawa na ummu't-tihala
ambaye watu wa nyumbani kwake mwenyewe walipendelea kuzini naye"
Haya ndio
maneno ya Abubakar akithibitisha kuwa Imam Ally amesalitiwa na watu wake na pia
akidai kuwa kulalamika kwake ni upumbavu mtupu kwa sababu hata afanyeje hawato
mrejeshea ukhalifa bali wataendelea kuwatesa Ahlulbayt mpaka wakubali kuwa
chini ya utawala wao wa haramu.
Comments
Post a Comment