UWAHABI NA FITINA ZAKE

Waislamu wa Madhehebu yote hapa Tanzania waliungana na kushirikiana pamoja bila kujali tofauti za kimadhehebu tangu zamani. Mfalakano na migogoro iliyopo baina ya waislamu hivi sasa imeletwa na Mawahhabi ambao ni wafuasi wa Muhammad Abdulwahab. Watu hawa huitwa vilevile kama Answari Sunnah na hivi karibuni wanajiita Salafi na wakati mwingine hujificha kwa kudai kuwa hawana madhehebu yoyote.
Wanazuoni mbalimbali wa kiislamu waliheshimiana na kushirikiana na walijiepusha na kutenda au kusema jambo lolote linaloweza kuleta mfarakano baina ya waislamu. Maibadhi, Masunni na Mashia waliishi kama ndugu na kushirikiana katika mambo ya dini. Maulamaa wa Kisunni kama vile allamah Sayyid Ahmed Sumeit walishiriki katika hafla za waislamu wa madhehebu mengine bila ubaguzi wowote. Lakini ujio wa Mawahhabi katika Tanzania umezua na kupanda mbegu mbaya za chuki baina ya waislamu, kwa kusambaza madai ya uongo kuwa watu wasiofuata Uwahhabi ni makafiri na kuhalalisha kuuwawa waislamu hao.
Ninamuomba Allah atuzindue waislamu tusije fuata fitna hizi za kiwahhabi na hivyo kuingia kwenye unafiki wa kuwafanyia uadui wanadamu wenzetu, sembuse waislamu kama wafanyavyo watu hawa wasiouelewa Uislamu.

Comments