As-Sayyid Ahmad ibn Zaini Dahlan, Mufti wa Makkah, akielezea katika somo la Al-fitnat al-Wahhabiyya (kitabu cha Al-Futuhat al-Islamiyya) kuhusu imani za Uwahhabi na dhuluma na maafa wanayoyapata Waislamu kutoka kwa Mawahhabi. Yeye anaandika: “Ili kutaka kuwadanganya ma’ulamaa wa Ahl as-Sunnah katika miji ya Makkah na Madinah, wao waliwatuma watu wao katika miji hiyo, lakini watu wao walishindwa kujibu maswali ya Maulamaa wa Kiislamu. Imekuwa dhahiri kuwa wao kwa hakika walikuwa ni wazushi majahili. Kulipitishwa sharia ikiwasema kuwa ni makafiri na kuenezwa kila mahala. Shariff Mas’ud ibn Sai’d, Amir wa Makkah, aliamrisha kuwa Mawahhabi watiwe mahabusu. Baadhi ya Mawahhabi walikimbilia Dar’iyya na kuelezea yale yaliyowapata.”
Maulamaa wa Hijaz, wanaotokana na Madhehebu yote manne, akiwemo Sulaiman ndugu yake Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab na waalimu wake waliokuwa wamemfundisha, walivisoma vitabu vya Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab na wakatayarisha katika sura ya vitabu majibu ya maandiko yake, yenye kuleta utenganishi na kuidhuru Islam, kwa ajili ya kuwatanabahisha Waislamu, wajitahadhari na kujitenga na upotoshi wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab.
Kwa hakika vitabu hivi havikuweza kusaidia zaidi na badala yake viliongeza hasira na chuki za Mawahhabi dhidi ya Waislamu na kumzuzua zaidi Muhammad ibn Sa'ud awashambulie Waislamu na kusababisha umwagikaji mwingi wa damu. Yeye alitokana na kabila la Bani Hanifa, kabila ambalo alitokamo mzushi wa Utume Musailamat al-Kadh-dhab. Muhammad ibn Sa'ud alikufa katika mwaka 1178 (1765), na hivyo kwa mujibu wa katiba waliyokuwa wametunga, mwanake ‘Abd al-‘Aziz alimrithi. ‘Abd al-‘Aziz aliuawa kwa kupigwa kisu tumboni, katika msikiti wa Dar’iyya katika mwaka 1217 (1803). Na hapo mtoto wake Sa’ud ibn ‘Abd al-‘Aziz ndiye aliyekuwa chifu wa Mawahhabi. Hawa wote watatu walijitolea kimabavu kama kwamba walikuwa wakishindana, katika kumwaga damu ya Waislamu ili waweze kuwadanganya na kuwapotosha Waarabu na kueneza Uwahhabi.
Comments
Post a Comment