at-Tarikhat-Tabari,
chapa ya Leiden (ya mwaka 1879 Miladia) kimeyanakili maneno ya Mtukufu
Mtume (s.a.w.w) aliyoyatumia wakati wa karamu mashuhuri ya ndugu wa karibu
aliyoitayarisha ambapo katika khutba yake alisema: “Enyi watu wangu! Huyu Ali
ni ndugu yangu, Wasii wangu na Khalifa wangu miongoni mwenu; msikilizeni na
mtiini.” Lakini katika chapa ya Misri ya mwaka 1963, (chapa inayodaiwa kuwa
imechekiwa na ile ya Leiden) maneno haya muhimu: “Wasii wangu na Khalifa wangu”
yamebadilishwa na kuandikwa “kadha wa kadha” na kusomeka hivi: “Huyu Ali ni
ndugu yangu na kadha wa kadha.”
Huu ni msiba mkubwa. Huu ni mchezo umefanywa na
unaendelea kufanywa mpaka leo. Na lengo ni kuficha ukweli. Lakini hata hivyo,
‘ukweli siku zote unaelea’; matoleo ya zamani yapo mengi na yamehifadhiwa
kwenye maktaba zetu.
Ni muhimu kufikia kila aina ya maoni katika kujaribu
kuamua ukweli.
Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa.
Utafiti huu umefanywa ili kuwaelemisha Waislamu kwa ujumla juu ya madhehebu za
Kiislamu ili kujenga maoni yao kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe, na ni muhimu
mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inawezekana kusemwa kwamba wale
ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu
(mtazamo) wa kwao wenyewe.
Hivyo tuendelee kufanya utafiti na tumwombe Allah
atuonyesha haki kuwa hii ni haki aturuzuku kuifuata na pia atuonyeshe bayana
kuwa hii ni batili na atuepushe kuiacha. Jibu ameen.
Comments
Post a Comment