WAPO WATU WANASEMA KUWA KHERI NA SHARI HUTOKA KWA MUNGU, JE KUNA UKWELI GANI WA HILO?

Ukweli ni kuwa, kwa Mungu hakutoki shari hata kiduchu jamani.
Kwa Mungu jamani kunatoka kheri tupu.
Mungu ni mwema zaidi ya unavyoweza kumtaja. Ni hapo ndipo hata wanadamu katika kujaribu kudhihirisha wema wake Mungu wakasikika wakisema; Mungu hamtupi mja wake. Mara wakasikika wakisema: Mungu si athumani. Mara wakasema: Mungu ni Mwema nk. Maneno yote hayo yanawakilisha hisia za mwanadamu juu ya wema wake Mungu.
Aidha ni kwamba, duniani hakuna kitu kinachoitwa shari. Na hata ukiangalia hapo ulipo, tafakari mwanzo hadi mwisho utafute shari unayoijua wewe iliyowahi kukupata, tafuta kamwe hutaipata.
Na kama utaipata basi mimi nitakunyooshea mikono ya heshima na nitakuwa mwongo.
Kila jambo lolote unaloliona ni shari, basi sio shari bali ni kheri ambayo wewe hufahamu matokeo yake. Mara nyingi ili Mungu akufikishe katika kilele cha mafanikio nk, hukupa mtihani ambao wewe utauona ni shari, lakini ukweli ni mtihani kuelekea kheri. Hii inafanana na mwalimu au mzazi anayemchama mwanaye ili kumuandaa kufikia utukufu. Hapo hatutaweza kusema kuwa kichapo kile ni shari, laa hasha, hatakama mtoto atalia na kusaga meno, lakini mzazi au mwalimu yule anajua kuwa, hiyo ndio njia kufikia mafanikio yake mtoto yule.
Kwamfano nyumba ya ghorofa imeanguka watu wakafa, je hiyo ni shari?
Au kwamfano nimechukua kisu nikakuchoma nacho ukafa, je utasema kisu ni shari?
Au tuseme mtu ameungua kwa moto akafa, je utasema moto ni shari?
Au mtu amekupiga bastola ukafa, je utasema bastola ni shari?
Au umepita porini ukakamatwa na simba au chuwi wakakutafuna, je utasema simba au chui ni shari?
Au umevuka mto au ukaogelea ziwani au baharini, ukatafunwa na mamba au samaki mkubwa, je tutasema mamba au samaki huyo ni shari?
Au kwamfano uko ndani ya meli au mashua ama boti, na ikazama na watu wakafa, je tutasema meli, boti au mashua ni shari?
Au tujengee unasafiri ndani ya ndege, ikaanguka na ukateketea humo je tutasema ndege ni shari?
Au umepanda gari, baiskeli, trein, pikipiki na vikapata ajali, je tutasema, trein, gari, pikipiku au baiskeli ni shari?
Au umeoa mke au umeolewa, na mara mpenzi wako akakugeuka na akakuua je tutasema mume au mke ni shari?
Au umekula sumu na ukafa, je ile sumu tutasema ni shari?
Au umekula madawa kwa nia njema ukafa, je madawa nayo yatakuwa shari?
Au wale wanaomeza madawa mengi ili waavye mimba (waporomoe mimba) je tutasema madawa yale ni shari?
Au dereva wa usafiri fulani ameendesha kwa uzembe na akapelekea kuua watu, je dereva ni shari? Au je aliyesababisha ajali hiyo ni Mungu hata tuseme shari imetoka kwake?
Na kadhalika pia pia pia pia
Yote hayo yanaonyesha wazi kwamba, hakuna kitu hata kimoja ambacho ni shari hata kidogo? Bali kinyume chake vyote hivyo nilivyovitaja na ambavyo sikuvitaja, ni kheri tupu. Tena bali zaidi ni kwamba hata Kifo chenyewe ambacho kiumbe anakiogopa, Mungu anakizungumzia kwa kusema kuwa; Mmelazimishiwa vita ilhali ni karaha kwenu. Huwenda mkakipenda kitu, kikawa shari kwenu. Na huwenda mkakichukia kitu, nacho, kikawa kheri kwenu.
Kwahiyo duniani hakuna shari kabisa. Na kama yupo anayejua shari yoyote basi aitaje hapa.
Mungu ni mwema tu, na kamwe hajawahi kumfanyia kiumbe wake shari yoyote, bali shari unayoijua, inatoka kwa viumbe wenyewe. Itakuwaje wewe unichome kisu kisha nife, alafu useme ni shari imetoka kwa Mungu?
Umepita porini Mikumi, simba wamekuchangamkia, itakuwaje useme ni shari imetoka kwa Mungu na wakati mwenyewe umetakiwa kutopita kwa mguu pori hilo?
Umeogelea ktk mto wenye mamba, umetafunwa, iweje useme ni shari ya Mungu?
Watu wamechakachua katika ujenzi wa nyumba kisha ikaporomoka na kuua watu, iweje useme ni shari kutoka kwa Mungu?
Dereva amezembea barabarani ameua watu, iweje tuseme ni shari ya Mungu, ilhali tukimkamata huyo huyo dereva tunampandisha kizimbani kwa kuua? Kama ni shari ya Mungu mbona tumpandishe kizimbani?
Meli imezama kwa sababu mbalimbali kama vile, mzigo mkubwa, au kutoboka, au kwa mawimbi, au kwa uzembe wa kapteni, je utasemaje ni shari ya Mungu? Mzinzi au mtu yeyote amefanya mahusiano na mtu mwathirika, kisha akaathirika na yeye pia, itakuwaje useme ni shari imetoka kwa Mungu ilhali alikuwa anaouezo wa kuachana na jambo hilo kabla? Hii leo walimwengu wamechafua mazingira na kuharibu utando wa Ozon, jambo lililosababisha kuongezeka majanga kama vile, mafuriko, uyeyukaji wa barafu baharini na kufanya maeneo kavu kumezwa na maji ya bahari, kuongezeka joto kali, kuharibika kabisa mlingano wa maisha bora duniani, je utasema ni shari imetokea kwa Mungu ilhali kila siku nchi tajiri huwa zinatakiwa kupunguza viwanda vyake ili kupunguza myoshi inayokwenda kuharibu Ozon?
Yanapokuja mafuriko, au Tsunami, au ukame au joto kali na kuua watu, bado utamlaumu Mungu?
Nani wa kulaumiwa, Mungu au mwanadamu mwenyewe?
Jamani jamani jamani, tuache kumsingizia Mungu. Tusome sana dini na falsafa ambayo kwa baadhi ya watu kutoisoma ndio wakafikia kumsingizia Mungu bure.nisawa na kusema kama huko mwanzo kwa nn mungu atuhukum na hali ya kuwa yeye mwenyewe katuumba au atufishe hali ametuumba je lengo lake lilikuwa ni hili basi kulikuwa hakuna faida ya kutuumba.kipande hiki nakibakisha wakati ujao tutakijadili palipo na majaliwa ishaallah.

Comments