WATOTO WA MTUME MUHAMMAD (S.AW).

Watoto wake ni kama wafuatao:  1- Abdallah.  2- Qaasim.  3- Ibrahiim (a.s)  4- Fatimatuz  zahraa (a.s). na kuna kauli zingine zisemazo kuwa  Zainab, Ruqayya, na Ummu Kulthum  ni wanawe pia (lakini watu hawa sio watoto wake bali aliwalea kutokana na mzazi wao alikuwa ni ndugu wa mke wake kipenzi bi Khadija bint Khuwalid).

Watoto wake wa kuzaa wote walikufa kabla ya kufikia utu uzima, isipokuwa mtoto mmoja tu ambaye anaitwa Fatma bint Rasulullah (s.a.w.w). bint huyu Mtukufu ndiye aliyekusudiwa na Allah katika Surat Kawthar baada ya makafiri kumshutumu Mtume (s.a.w.w) kuwa ni tasa kutokana na watoto wake wa kiume wote kufariki dunia.

Comments

Post a Comment