Mtume (s.a.w) ali walingania watu
kwenye upweke wa Mwenyezi Mungu katika mji wa makka na kwa njia ya siri
kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kipindi cha siri ali waita watu kwa njia
ya wazi kwa muda wa miaka kumi.
KUHAMA KWAKE.
Alihama kutoka katika mji wa makka kwenda madina
mwanzoni mwa mwezi wa rabiul awwal baada ya kupita miaka 13 tangu
kupewa utume, na kuhama huko kulitokana na maudhi mengi ya makuraishi,
mushrikina na mkafiri kumuelekea yeye na maswahaba wake. Kiasi kwamba
maswahabi wengi waliuawa na makafiri wa kikuraishi kiasi kwamba alilazimika
kuwatorosha waislamu na kuwapeleka Ethiopia ili wapishe mateso na dhuluma
wanazofanyiwa na makafiri wa Maka. Walioteswa sio Masahaba pekee bali hata yeye
mwenyewe na familia yake.
Ukoo wa Mtume (s.a.w.w) uliwahi kuwekewa vikwazo
kwa muda wa miaka mitatu kiasi kwamba walifukuza mjini Maka na kwenda kuisha katika pango la Abutalib kiasi
kwamba hawakuruhusiwa kuuza kitu wala kununua na wala hawakuruhusiwa kuingia
mjini. Utakumbuka vilevile kuwa siku moja alifunga safari kwenda katika mji wa
jirani iitwao Taif na huku alikuta watu wamejipanga mistari na kumshambulia kwa
kila silaha na kulazimu kurudi Maka bila kufanya tabligh katika mji huo.
Wale wanaosema kuwa Uislamu unaenezwa kwa nguvu
wamekosea sana. Uislamu unaenezwa kwa mahubiri tu. Kama ingekuwa utumiaji nguvu
kuutangaza Uislamu linaruhusiwa katika Uislamu basi tungeshuhudia Mtume
akipambana na watu kuwalazimisha waingie katika Uislamu. Kama watu
walilazimishwa kuukubali Uislamu basi hilo lilifanywa na madikteta walionyakua
utawala wa dini ya Kiislamu na kuugeuza kuwa ni ufalme. Na Qur’an inatuambia
bayana kuwa wafalme wakiingia katika miji huiharibu miji hiyo na kuwadhalilisha
wakazi wa miji hiyo. Hiyo ndio kazi iliyofanywa na watu waliopora madaraka
ndani ya Uislamu na kuwachinja wengi sio tu wa wasiokuwa waislamu bali
waliwachinja waislamu wengi zaidi kuliko wasiokuwa waislamu.
Kazi hii ya ufedhuli inaendelezwa na maadui wa
Allah waitwao Mawahhabi ambao wameshamirisha vita zao za kiibirisi na
kuwachinja na kuwalipua watu katika dunia nzima.
Comments
Post a Comment