Wakati Mtume alipokuwa akirejea kutoka Hijja yake ya mwisho wa uhai wake, alisemama katika eneo liitwalo Khum, kati ya Makkah na Madinah, akasema Ali alikuwa ndiye khalifa wake na mwenye kutawala mambo yote ya waumini.
Tukio hili limeandikwa na waandishi wengi wa kisunni. Imam Ahmad bin Shu'ayb an-Nasai amesimulia tukio hili kupitia sanad (nyororo) mbali mbali za wasimuliaji wa hadithi katika kitabu chake al-Khasa'is, mojawapo ikiwa kama ifuatavyo:
Abu't-Tufayl alisema kwamba Zayd bin Arkam alisema, wakati Mtume (S.A.W) alipokuwa anarudi toka Hijja yake ya mwisho, akapumzika penye bwawa (Ghadeer) la Khum, aliagiza sehemu hiyo ifagiliwe. Kisha akasema; inaelekea kama vile nimeitwa (kurejea kwa Mola wangu) nami nimekubali wito huo. Nakuachieni miongoni mwenu vizito viwili vyenye thamani, kimoja ya hivyo ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Allah (s.w) na Ahlulbayt wangu (kizazi changu). Hivyo angalieni jinsi mtakavyojihusisha navyo baada yangu kwa sababu vitu hivyo havitatengana mpaka vitakapokuja kwangu kwenye chemchem (ya kawthar siku ya hukumu).
Kisha akaendelea kusema, mimi ni mwenye kuwatawalia (walii) mambo ya kila muumini. Wakati akisema hayo aliunyoosha mkono wa Imam Ally (a.s) na akasema, yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kumtawalia mambo yake, huyu (Ali) ni mwenye kumtawalia mambo yake pia.
(Kisha akaomba dua) akasema, Eewe Allah! Mpende mwenye kumpenda Ali, na uwe adui kwa kila mwenye kumfanyia uadui yeye.

Abu't-Tufayl anasema, nilimuuliza Zayd, maneno haya uliyasikia kutoka kwa Mtume wa Allah? Akasema, hakuna mtu aliyekuwa mahala pale, ila alimuona kwa macho yake na kumsikia kwa masikio yake.
Soma: An-Nasa'l, al-Khasa'is uk 15.
Comments
Post a Comment