Kwa
jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa ukarimu.
ZAKAAT kwa Kiarabu ni neno lenye maana mbili: (1)
kuongezeka, na (2) kutakasika. Katika
sheria ya Kiislamu maana yake ni kutoa sadaka sehemu
maalumu ya Mali liyoichuma Mwislamu kwa njia ya halali.
Kutoa Zaka ni nguzo ya katika nguzo tano za Kiislamu
kwa upande wa Sunni na pia ni tawi katika matawi ya dini kwa mujibu wa
Madhehebu sahihi zaidi katika Uislamu, nayo si nyingine bali Shia imamiya; na
kila Mwislamu, mwanamume
au mwanamke, akiwa na kipimo maalumu cha mali,
amelazimishwa kuitoa. Zaka imetajwa
pamoja na Sala ndani ya Kurani Tukufu na hilo
laonyesha jinsi ilivyo muhimu amri hii.
Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume Muhammad s.a.w.
kuchukua sadaka kwa Waislamu.
Akasema “Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe
kwayo na kuwatakasa, na uwaombee. Hakika kuomba kwako ni utulivu kwao; na
Mwenyezi Mungu ndiye Asikiaye, Ajuaye.” (9:103).
Baada ya kufariki Mtume s.a.w. Makhalifa wake
waliendelea kupokea sadaka hiyo kwa
Waislamu, na wakati mmoja baadhi ya Waislamu
walipokataa kutoa Zaka, Seyidna Abu Bakr, Khalifa wa kwanza wa Mtume kwa mujibu
wa Masunni, Mungu awe radhi naye, akawa tayari kupigana nao, akatangaza
kwamha hataacha kuwapiga vita watu hao mpaka watoe
kile kipande cha kamba cha kufungia goti la ngamia walichokuwa wakitoa zama za
Mtume s.a.w. Maana yake, Mwislamu ambaye anayo mali wala hatoi sehemu yake
iliyolazimishwa na Mwenyezi Mungu hawi Mwislamu tena
Tena amesema Mwenyezi Mungu, "Na kama wakitubu na
kusimamisha Sala na kutoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika dini" (9:11).
Bila shaka kutoa Zaka kunaimarisha udugu wa Uislamu, na mwenye kuitoa tu ndiye
ndugu ya Waislamu wengine.
Kutokana na hili Khalifa
wa Kiwahhabi Abubakar bin Quhafa (R.A) ALIWAUWA MASAHABA WENGI KWA KUGOMA
KULIPA ZAKA KWA SABABU YA KUTOUTAMBUA UONGOZI WAKE ULIOPATIKANA KIUTATA NA
UBABE KWA KUWATISHA WATU KUWAUA NA HAKIKA WALIWAUA BAADHI YAO. Mmoja wa walioua
ni Maliki ambapo kamanda wa majeshi ya Abubakar kwa kipindi hicho akiitwa Khalid
bin walidi alimbaka mjana wa Maliki jirani tu na maiti ya mme wa mama huyo. Huu
ni msiba mwingine ulioukumba uislamu kwa watawala kulazimisha twa’ toka kwa
waumini, hata pale ambapo hawakuistahili kwani tayari Mtume (s.a.w.w) aliache
amemtangaza Imam Ally kuwa khalifa wake wa kwanza.
Comments
Post a Comment