BAHLUL AJIBU SWALI KUTOKA KHALIFA HARUN.
Siku moja khalifa wa Mawahabi yaani, Harun
Rashid alikuwa katika Qasri yake akiangalia mandhari iliyokuwa ikimzunguka na sauti
ya mbubujiko wa maji ya mto Tigris.
Na mara hapo akatokezea Bahlul, na Harun
alimwambia Bahlul: "Ewe Bahlul! leo hii nakuuliza fumbo, iwapo utafumbua
vyema basi nitakupa dinar elfu moja na iwapo utashindwa basi nitatoa amri ya
kukutosa majini." Bahlul alimwambia Harun: "Mimi sihitaji dinar hizo,
bali ninakubali kwa sharti moja." Na alipokubali Harun, Bahlul alisema:
"Iwapo nitaweza kulijibu vyema basi itakubidi kuwaachia (Mashia) marafiki
zangu mia moja - kutoka Gereza lako, na iwapo nitashindwa basi unao uhuru wa
kunitupa majini."
Alianza Harun kulielezea fumbo lake:
"Iwapo mimi ninaye mbuzi mmoja, mbwamwitu, na fungu la majani.Je nitawezaje
kuvivusha vyote hivyo, kwamba majani hayataliwa na mbuzi na wala mbuzi kuvamiwa
na mbwamwitu?"
Bahlul alianza kumjibu: "Kwanza
utamvusha mbuzi kwenda ng'ambo ukimwacha mbwa mwitu na majani. Baadaye
utachukuwa majani uyavushe huku ukirudi na mbuzi upande huu. Utamwacha mbuzi
upande huu na utamchukua mbwamwitu ng'ambo. Mwishoni utampeleka mbuzi. Kwa hivi
majani hayataliwa na mbuzi wala mbuzi kuvamiwa na mbwamwitu."
Harun alifurahishwa mno kwa majibu ya
Bahlul. Na hapo Bahlul alimpa orodha ya majina mia moja ya wafuasi na wapenzi
wa Ali bin Abi Talib (a.s. ).
Lakini Harun alimgeuka Bahlul na akagoma
kuwaachia huru Mashia waliokuwa wamejaa magereza. Kwa upande wake, Bahlul
aliendelea kusisitiza, na hatimaye aliwaacha huru watu kumi tu na akimwamwuru
Bahlul kuondoka.
FUNDISHO.
1. Baada ya Mtume (s.a.w.w) kufariki
wafuasi wake na wafuasi wa khalifa aliyemteua kuongoza baada yake yaani imam
Ally (a.s) waliteswa, kufungwa na kuawa na watawala waliodai kuwa wao ndio
makhalifa hasa. Hii ndio sababu ya Mashia kuwa wachache kwani mpaka leo wafuasi
wa makhalifa hao waovu hawaridhiki mpaka wao ndio wawe watawala, na
wanapotawala kazi zao ni kuwauwa waislamu wasio na hatia maadamu wanatofautiana
nao kimtazamo.
2. Makhalifa hao walikuwa ni wanafiki
kwa sababu ukichukulia mfano wa Harun Rashid katika tukio hili alitoa ahadi, na
Allah katika Qur’an anatuambia ahadi lazima itimizwe na siku ya kiama utaulizwa
lakini hakujali na akamdanya Bahlul kama ulivyosoma mwenyewe.
3. Waislamu tuendelee kuusoma Uislamu
kwa undani ili tuwe pamoja na wakweli na kujiepusha na kundi la waovu
waliowafunga na kunyonga mashia na waislamu wengine waliotofautiana nao
kimtazamo. Kumbuka suala la kutofautiana wanadamu ni la kimaumbile na hakuna sababu
ya kuuana.
Comments
Post a Comment