BAHLUL AUZA PEPO

BAHLUL AUZA PEPO
Siku moja Bahlul alikuwa ukingoni mwa mto akicheza kwa udongo kwa kutengeneza nyumba na bustani.

Hapo alitokea Zubeidah, mke wake Harun Rashid (khalifa wa Mawahhabi na Masalafi), akipita hapo. Alipomkaribia Bahlul, alimwuliza: "Ewe Bahlul! Je wafanya nini?" Bahlul alimjibu: "Najenga Pepo (Jannat)."
Zubeidah alimwambia: "Je wauza hizi Pepo ulizozijenga?" Bahlul alimjibu: "Naam ninaziuza!" Zubeidah alimwuliza: "Je kwa Dinar ngapi?" Bahlul alimjibu "Kwa Dinar mia moja tu!"

Kwa kuwa Zubeidah alikuwa akitaka kumsaidia Bahlul, hivyo aliona hapo ndipo pahala pa kumsaidia na alimwamuru mfanyakazi wake amlipe Bahlul hizo fedha. Nao walimlipa hizo
dinar mia moja.

Usiku ule Zubeidah aliota ndoto akiwa Peponi ambamo kuna Qasri nzuri mno iliyopambwa mno na wapo wajakazi wamesubiri amri, wao walimwambia hiyo ndiyo Qasri aliyoinunua kutoka kwa Bahlul. Zubeidah alipoamka siku ya pili, akiwa amejawa na furaha, alimwelezea mume wake,

Harun. Harun alimwita Bahlul, alipofika, Harun alimwambia, "Ewe Bahlul, chukua hizi Dinar mia moja na uniuzie Pepo mojawapo ya Pepo kama ile uliyomwuzia Zubeidah."

Bahlul alicheka na kumwambia: "Zubeidah alinunua bila ya kuona ambapo wewe unataka kununua baada ya kujua ya kuwapo kwake. Hivyo sitakuuzia!"

MAZINGATIO.
1.Mtu mwovu anaweza kuwa na mke au mme mcha Mungu. Hivyo asihukumiwe mtu kwa sababu ya mkosa ya ndugu yake au rafiki yake. Harun Rashid pamoja na kuwa alikuwa mwovu aliyepindukia hasa kwa kuwaua waislamu wafuasi wa Mtume na Ahlulbayt wake (Mashia) lakini alikuwa na mke mwislamu sahihi aliyekuwa na huruma na wanadamu wote ikiwemo Mashia.
2. Imani ya kidini imejengwa juu ya kuamini mambo yasiyoonekana. Hivyo ukijifanya wewe ni myakinifu, unataka uone kitu ndipo ukiamini basi dini itakushinda. Tunatakiwa tusikiapo jambo la dini tuhoji kusihi kwake na tukiridhika tufuate mara moja hata kama halionekani.itakuta baadhi ya watu tukiwaambia Allah haonekani wanakuwa wakali na kudai kuwa ni lazima aonekane. Hawa wanafanana na Harun Rashid

Comments