HADITH YA MTUME IITWAYO HADITH YA KARATASI
Hii ni Hadith iliyo mashuhuri sana. Wanazuoni wa
Hadith wameitaja katika vitabu vyao, na vile vile wanahistoria kadha wa kadha
wameitaja katika vitabu vyao. Na kati ya wote hao hakuna hata mmoja aliyelikanusha
tukio hilo, wala kulitilia shaka.
Kati ya vitabu vya Hadith vilivyosimulia kisa
hiki ni Sahih Bukhari Kwa masunni, hiki ndicho kitabu kilicho
sahihi mno, na kwa hivyo kuaminiwa mno, baada ya Qur'ani Tukufu. Katika kitabu hicho muna riwaya sabaa zinazosimulia
kisa hicho. Kwa faida ya wasomaji wetu, hapa chini tunazidondoa zote:
1. Imepokewa kwa Ibn Abbas akisema:"Mtume (s.a.w.w.)
alipozidiwa na maradhi yake, alisema: Nileteeni (karatasi ya) kuandikia,
niwaandikie maneno ambayo baada yake hamtapotea. Lakini Umar akasema: Hakika
Mtume (s.a.w.w.) amezidiwa na maradhi, na sisi tunacho Kitabu cha
Mwenyezi Mungu. Kinatutosha. Hapo basi (maswahaba) wakakhitalifiana,
na zogo likazidi, (Mtume s.a.w.w.) akasema: Niondokeeni! Haifai kuzozana mbele
yangu."
Ibn Abbas akatoka huku anasema: "Msiba
ulioje wa Mtume (s.a.w.w.) kuzuiwa kuandika (alichotaka kuandika)."
Hadith hii imo katika Kitaabul Ilm, Mlango
wa
Kitaabatil Ilm. Kwa
tafsiri ya Kiingereza ya kitabu hicho, ni Hadith Na. 114, uk. 86 wa Juzuu ya
Kwanza.
2. Imepokewa kwa Said b. Jubayr kwamba alimsikia
Ibn Abbas (r.a.) akisema: "Siku ya Alkhamisil. Na ni ipi hiyo siku ya Alkhamisi?"
Kisha akalia mpaka mawe yakaloa kwa machozi yake. Nikamuuliza: "Ewe Ibn
Abbas! Ina nini hiyo siku ya Alkhamisi?" Akasema:
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alizidiwa na
maradhi yake. Akasema: Nileteeni mfupa wa bega niwaandikieni maneno ambayo
baada yake hamutapotea abadan. (Maswahaba) hapo wakazozana, wala haifai kuzozana
mbele ya Mtume s.a.w.w. Na wakauliza: Ana nini? Anaweweseka? Muulizeni
(ili mujue hali yake). Mtume (s.a.w.w.) akasema: Niacheni! Niliyonayo ni bora
kuliko hayo munayonitaka nyinyi niyafanye.
"Hapo (Mtume s.a .. w.w.) akawaamrisha
mambo matatu. Akasema: Watoeni Bara Arabu washirikina wote, wapeni
zawadi wajumbe (wa kigeni wanapokuja kwenu) kama nilivyokuwa nikiwapa mimi.
Msimuliaji akaongeza: "La tatu ni jambo la kheri ambalo ama Ibn Abbas
alilinyamaza, au alilitaja lakini nimelisahau!"
Hadith hii imo katika Kitaabu Fardhil
Khumsi:
Mlango wa Ikhraajil Yahudi Min Jaziratil
Arab. Kwa Kiingereza ni Hadith No. 393, uk. 260 wa Juzuu ya Nne.
3. Maneno ya hii Hadith ya tatu karibu yote ni
sawa na yale ya Hadith No.2 hapo juu. Nayo imo katika Kitaabul
Maghaazil: Mlango wa Maradhin Nabiyyi (s.a.w.w.) wa Wafaatihii: Kwa
Kiingereza, ni Hadith Na. 716, uk. 511 wa Juzuu yo Tano.
4. Imepokewa kwa Ubaydullah kwamba Ibn Abbas r.a.
amesema:"Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alipouguwa maradhi ambayo ndiyo
aliyofia, na nyumbani mwake mkawa mna watu akiwamo Umar miongoni mwao, alisema:
Njooni niwaandikie maneno ambayo hamutapotea baada yake. Umar akasema:
Hakika Mtume s.a.w.w. amezidiwa na maradhi (anaweweseka), na
nyinyi munayo Qur'an: Kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Watu
waliokuwapo hapo nyumbani wakazozana. Wengine walisema: Njooni karibu ili Mtume
(s.a.w.w.) awaandikie maneno ambayo hamutapotea baada yake. Na wengine wakasema
alivyosema Umar. Walipozidisha zogo lao na ikhtilafu zao mbele ya Mtume
s.a.w.w., Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: Niondokeeni!
"Ubaydullah anasema: Ibn Abbas alikuwa
akisema: Msiba ulioje wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuzuiwa kuyaandika
maneno haya kwa sababu ya ikhtilafu zao na zogo lao."
Hadith hii imo katika Kitaabul
Mardhwaa, Mlango wa Qawlil Mariidhwi Quumuu Annii. Kwa
Kiingereza ni Hadith Na. 573, uk. 389 wa Juzuu ya Sabaa.
5. Maneno ya hii Hadith ya tano karibu yote ni
sawa na yale ya Hadith Na. 4 hapo juu. Nayo imo katika Kitaabul
I'tiswaami Bil Kitaabi was Sunnah, Mlango wa Karaahiyatil
Ikhtilaaf Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 468, uk. 346-347 wa Juzuu ya
Tisa.
Hii ndio Historia ya Uislamu na matendo ya baadhi
ya maswahaba kwa Mtume wetu, nadhani kwa kuhofia kujulikana kwa ukweli huu,
kutawapa watu mwanya wa kuujua Uislamu sahihi basi wameamua wafuasi wao kudai
kuwa ni makosa kusoma historia ya Uislamu kwa ukamilifu bali soma yale watakayo
wao tu ambayo kwa hakika yamechakachuliwa na kupata sifa za viongozi wao na
kuondoa uhalisia wa Historia yenyewe.
Ukiendelea kufuatilia kisa hiki utagundua kuwa
Umar aliogopa kutangazwa Khalifa kwa mara nyingine, kwa sababu alijua wazi kuwa
khalifa anayetakiwa na Mtume ni Imam Ally (a.s). Hivyo ili kufanikiwa njama zao
dhidi ya Uislamu na waislamu aliona ni bora kuwazuia waislamu kukumbushwa
Ukhalifa wa Ahlulbayt (a.s).
Comments
Post a Comment