ITIKADI YA SHIA ITHNA ASHARIA KUHUSU SIFA TUKUFU ZA KIJALALI NA KIJAMALA ZA ALLAH (S.W).

ITIKADI YA SHIA ITHNA ASHARIA KUHUSU SIFA TUKUFU ZA KIJALALI NA KIJAMALA ZA ALLAH (S.W).
Sisi tuna itikadi ya kuwa; Mwenyeezi Mungu (s.w) ametakasika na kila aibu, Mwenyezi Mungu ni mkamilifu wa kila kitu, kwa maelezo mengine, kila jema, na kila kamilifu liliopo katika ulimwengu huu linatokana na dhati iliyotakasika yake Yeye Allah (s.w).

Qur’an takatifu imeandika, “Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo.
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilichoko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hekima (Surat Al-Hashr Aya ya 23-24).

Maelezo kuhusiana na Aya:
Aya hizo zinataja sifa nyingi za Mwenyeezi Mungu, sifa ambazo zimeelezewa fadhila zake katika hadithi nyingi za Mtume Muhammad
 (s.a.w.w).

Tutaendelea kuleta mada kuhusu Allah mtakatifu na kuonyesha wazi kuwa Mawahhabi hawamtambui Allah (s.w) vilivyo, huenda ujinga wao ndio unaowasababisha kuwauwa watu wasiokuwa na hatia kwa madai ya ushirikina.

Kama sisi tungekuwa na tabia mbaya kama wao basi tungewaangamiza kwa sababu hakika wao ndio makafiri kwa sababu washirikina.

Kama sisi tungekuwa na tabia mbaya kama wao basi tungewaangamiza kwa sababu hakika wao ndio makafiri kwa sababu wanamnasibisha Allah na viumbe vyake. Hakuna tofauti ya Mawahabi na wakristo kwa sababu wote wanaamini kuwa Mungu ana miguu, husafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine, ana mikono, ana macho n.k. Allah ametakasika kutokana na sifa hizi zenye mapungufu ya kibinadamu. 

Comments