ITIKADI YA SHIA ITHNA ASHARIA KUHUSU DHATI YA ALLAH (S.W) IMETAKASIKANA ISIYOKUWA NA MWISHO.

ITIKADI YA SHIA ITHNA ASHARIA KUHUSU DHATI YA ALLAH (S.W) IMETAKASIKANA ISIYOKUWA NA MWISHO.
Sisi tunaamini kuwa dhati  ya Mwenyeezi Mungu imeenea sehemu zote, naye hana mwanzo wala mwisho, dhati hiyo inaonekana katika elimu yake, qudra ya utukufu wake, kubakia kwake milele katika sehemu zote na zama zote, na kwa sababu hiyo basi ndio tukasema kuwa Mwenyeezi Mungu hana sehemu maalumu wala kipindi maalumu, kwa sababu sehemu au nafasi na zama zina kiwango maalumu, japokuwa Mwenyeezi Mungu hana sehemu maalumu wala zama maalumu lakini Yeye yuko katika sehemu na zama zote, kwa sababu dhati ya utukufu wake ni iko juu zaidi kuliko sehemu na zama, kama tunavyosoma ndani ya Qur-an:-
Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi 5.

Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika nyakati sita; kisha akakaa vyema juu ya enzi. Anayajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni, na yanayo panda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayo yatenda6.

Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitia katika nafsi yake7Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
Maelezo yanayopatikana katika Aya hiyo.

Rejea:
[5] Surat Az-Zukhruf Aya ya 84
[6] Surat Al-Hadiyd Aya ya 4

[7] Surat Qaf Aya ya 16

Comments