ITIKADI YA SHIA JUU YA UTUME NA MITUME WA ALLAH (S.W).

ITIKADI YA SHIA JUU YA UTUME NA MITUME WA ALLAH (S.W).
Sisi tuna amini ya kuwa ; Mwenyeezi Mungu amewateremsha Mitume wake ili kuwaongoza na kuwafikisha wanaadamu katika ukamilifu na saada, kama Mwenyeezi Mungu asingewatuma Mitume kwa waja wake basi kusingelikuwa na madhumuni yoyote katika uumbaji wake, na wanadamu wasingeliweza kuongoka na kufikia katika saada.
Allah anasema katika Qur’an tukufu, “Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima”.
Sisi tuna itakidi ya kuwa; miongoni mwa Mitume hao, kuna Mitume mitano ambayo wanajulikanwa kuwa ni “Uulil-Adhimi” yaani ni Mitume walioteremshiwa vitabu vitukufu vya Mwenyeezi Mungu, Mtume wa mwanzo miongoni mwa Mitume hao wataano ni Nabii Nuhu (a.s), na baadae Nabii Ibrahimu (a.s), Nabii Mussa (a.s), Nabii Issa (a.s) yaani Yesu, na Mtume wa mwisho ambaye ni Nabii Muhammad (s.a.w.w).

Allah (s.w) anaendelea kusema, “Na tulipo chukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu” Surat Al-Ahzaab Aya ya 7.

Kisha anasema, “Basi subiri, kama walivyo subiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayo yaona waliyo ahidiwa itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine, walio waovu tu? (Surat Al-Ahqaaf Aya ya 35)


Comments