JE ABUBAKAR ALIONGOZA
SWALA WAKATI WA MTUME?
Imepokewa kwa mama wa waumini Aisha
kuwa, Mtume (s.a.w.) alipougua maradhi aliyofia, aliamrisha kuwa: Abubakr asalishe
watu, mimi (Aisha) nikasema, Abubakr ni mtu mpole sana, atakaposimama mahala
pako atashindwa (kusalisha) Mtume akaamuru: Abubakr asalishe. Nikasema kama
nilivyosema kwanza, Mtume akakasirika akasema: Nyinyi ni watu wa Yusuf.
Mara Mtume akahisi woga moyoni
mwake, akatoka akichechemea kwa kushikiliwa na watu wawili (Ali na Abbas)
alipofika Msikitini, Abubakr akarudi nyuma katika safu ya kwanza. Mtume akakaa
kuongoza swala, Abubakr akawa anafuata sala ya Mtume (s.a.w.) na Waislamu
wakawa wanapokea kwa Abubakr."
Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 439
Afatu As'habil Hadithi Uk. 13-30
Hapa pana mambo matano yanahitaji
kuangaliwa:
(a) Abubakr ni katika watu
walioamriwa na Mtume kutoka pamoja na jeshi Ia Usama bin Zaid. Kwa hiyo basi,
amma Abubakr alikwenda pamoja na jeshi hilo, na kwa hivyo hakusalisha maana
hakuwepo. Amma alikuwapo mjini, kwa hivyo alipinga amri ya Mtume (s.a.w.) na
kwa hivyo Abubakr amelaaniwa.
(b) Mtume (s.a.w.) alipougua maradhi
aliyofia, alikuwa ndani ya nyumba ya Mwana Aisha, Mtume alisema: "Niitieni
Ali" Aisha akajibu: "Laiti ungemwitisha Abubakr" Hafsa (mtoto wa
Umar) akasema: "Laiti ungemwitisha Umar" (kila mmoja akamwita baba
yake) wakakusanyika mbele ya Mtume. Alipowaona Mtume akawaambia "Ondokeni
nikikuhitajini nitakuiteni". Taz: Tarikhut Tabari J.3 Uk. 439.
(c) Mtume (s.a.w.) alipowaambia Aisha na Hafsa, "Nyinyi ni watu wa Yusufu" hapa inaonyesha kuwa amri ya kusalisha Abubakr si ya Mtume (s.a.w.), hali ya kisa cha wanawake waliomtaka Nabii Yusufu (a.s.) na yeye akajizia, na kisa cha Aisha na Hafsa kuwatanguliza mbele baba zao ni jambo lililofanana.
(c) Mtume (s.a.w.) alipowaambia Aisha na Hafsa, "Nyinyi ni watu wa Yusufu" hapa inaonyesha kuwa amri ya kusalisha Abubakr si ya Mtume (s.a.w.), hali ya kisa cha wanawake waliomtaka Nabii Yusufu (a.s.) na yeye akajizia, na kisa cha Aisha na Hafsa kuwatanguliza mbele baba zao ni jambo lililofanana.
(d) Mtume (s.a.w.) alitoka
akichechemea taabani na watu wawili wamemshikilia, Abubakr akapisha mahala
hapo, na Mtume (s.a.w.) akashika mwenyewe kusalisha. Ni jambo gani
lililomlazimisha kutoka akiwa hali hii, ikiwa yeye ndiye aliye amuru Abubakr
asalishe? Jambo gani lililomsonga asalishe watu hali amekaa chini kwa taabu na
dhiki kubwa?
(e) Kuonyesha dalili zote hizi,
haina maana kuwa: kama itasihi kuwa Abubakr amesalisha, basi itapasisha Abubakr
kushika uongozi baada ya kuondoka (kufa) Mtume (s.a.w.). Hii haina maana, kwa
sababu nafsi ya kusimama mbele na kusalisha watu si jambo lenye kima na thamani
tukufu ambalo litampasisha kupata kila apitae mbele na kusalisha watu!! Kwa
mujibu wa Hadithi za ndugu zetu Masunni, inasema kuwa: Mtume (s.a.w.) amesema,
"Salini nyuma ya kila mwema na muovu". Na kwa msingi huu Madhihabi ya
Imam Shaafy na Imam Ahmad na wengine wamepasisha Mwislamu asali nyuma ya yeyote
japokuwa Fasiq.
Taz: Assunanu Walmubtadiatu Uk. 182
Lakini pia tukiliangalia kwa wema suala hili
tunaona kuwa: Mtume (s.a.w.) alipokuwa akitoka kwenda vitani, nyuma alikuwa
akiweka mtu wakushika mahala pake katika masuala mbalimbali, ikiwa ni pamojana
kusalisha.
Comments
Post a Comment