JUA LAREJESHWA KWA AJILI YA IMAM ALLY (a.s)
Imeelezwa katika Marijun Nubuwah kwamba aliporejea
Mtume (s.a.w.w) kutoka Khaibar alipofika kwenye kituo “Sahba” baada ya kuswali
sala ya alasiri, Mtume akaweka kichwa chake kwenye miguu ya Ali (a.s) na
akalala.
Katika hali ya kulalal hali ya kutemshwa wahyi
ikadhihiri kwake na ikaendelea mpaka jua likazama. Ali (a.s) alikuwa hajaswali
swalatil asri. Ulipokwisha kushuka wahyi Mtume akamuuliza, Ali umeswali sala ya
alasiri? Imam Ali akajibu sikuswali, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume akaomba
kwa Mwenyezi Mungu, ‘ewe Mola, Ali alikuwa chini ya utii wako na utii wa Mtume
wako, inua jua tena ili aweze kusala sala ya alasiri’.
Mwenyezi Mungu hapo hapo akaikubali dua ya mpenzi wake;
Mtume, jua likachomoza tena (baada ya kuwa limekuchwa) na likatandaza mwangaza
nyikani na milimani. Watu wakashuhudia muujiza huu wa Mtume (s.a.w.w) kwa macho
yao. Kwa hiyo Ali akatawadha na kuswali.
Abu Jaafar al-Tahawi anaandika katika
Mishkil-ul-Athaar, hadith inayotokana na Asma bint Umair amesema, alipowasiri
Mtume kituo cha Sahba akaswali sala ya adhuhuri, tena akamtuma Ali kwa kazi ya
dharura, aliporejea Ali, Mtume alikuwa amekwisha swali Alasiri. Mara Ali
alipofika Mtume (s.a.w.w) akajilaza juu ya miguu ya Imam Ali (a.s) na akalala
mpaka jua lilipokuchwa. Alipoamka na akaarifiwa kuwa Ali hakusali alasiri.
Mtume (s.a.w.w) aliomba dua kwa Allah (s.w) akisema, “Mola wangu, Mtumwa wako
Mahsusi Ali amejitolea nafsi yake kwa ajili ya Mtume wako, tafadhali rejesha
jua lichomoze tena kwa ajili yake”.
Asma akaongeza kusema, ghafla jua likachomoza na
mwangaza wake ukaangaza juu ya ardhi na milima, Ali (a.s) akatawadha na kuswali
alasiri, kisha jua likazama tena.
Qadhi Ayadhi naye ameiandika hadith hii katika kitabu
chake kiitwacho Kitabush-Shifa.
Comments
Post a Comment