KHALIFA WA WAHABIA, HARUN RASHID AMKASIRIKIA BAHLUL

KHALIFA WA WAHABIA, HARUN RASHID AMKASIRIKIA BAHLUL
Harun alimwajiri jasusi makhususi kwa ajili ya kuchunguza na kuripoti kwake juu ya imani na akida sahihi za Bahlul. Baada ya siku chache huyo jasusi alikamilisha uchunguzi wake na kuripoti kwa Khalifa kuwa Bahlul alikuwa ni mpenzi wa Ahlal-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) na alikuwa mfuasi wa Imam Musa al-Kadhim (a.s.) (imam wa saba wa Shia).

Harun alimwita Bahlul na kumwambia: "Ewe Bahlul! Mimi nimepata habari za kuaminika kuwa wewe ni mmojawapo wa wapenzi na wafuasi wakubwa wa Musa ibn Jaafar na hivyo unafanya kila jitihada za kudhihirisha na hivyo umejidhihirisha u mwehu ambapo sivyo ulivyo!"

Bahlul alimjibu: "Iwapo hivyo ndivyo ilivyo, je utanifanya nini?"
Kwa majibu hayo, Harun alighadhibika mno na kumwamuru Masrur, mfanyakazi wake, amvue nguo Bahlul akalishwe juu ya punda na kuzungushwa mjini na hatimaye kukatwa kichwa mbele yake Harun. Masrur, alitekeleza vile alivyoamrishwa na hatimaye kumleta mbele ya Harun katika hali hiyo ili aweze kuuawa.

Mara, hapo akatokezea Jaafer Barmaki ambaye kwa kuiona hali hiyo ya Bahlul alimwuliza sababu ya hali yake hiyo:
"Ewe Bahlul! Je umetenda kosa gani?" Bahlul alimjibu: "Kwa kuwa mimi nimesema ukweli, kwa hivyo Khalifa akanizawadia mavazi yenye thamani."

Harun Rashid, Jaafar, na wote waliokuwepo walichekeshwa mno kwa majibu ya Bahlul, na papo hapo Harun alimsamehe Bahlul na kutoa amri ya kufunguliwa na apewe mavazi mapya na mazuri. Lakini Bahlul hakukubali hayo bali yeye alichukua kifurushi cha nguo zake kuukuu na kuondoka.

MAZINGATIO
1.  Watu wenye kudai kuwa ni waislamu lakini kazi zao ni kuwaua waislamu sio mawahhabi pekee bali hata zamani walikuwepo. Na Mtume na Ahlulbayt wake na wafuasi wao waliteswa sana na watu hawa ambao ni wanafiki lakini wanalazimisha kuwaongoza waislamu kwa nguvu.
2.  Ukiwa mwislamu wa kweli unapigwa vita kutoka pande zote ndani ya Uislamu na nje ya Uislamu. Hivyo kunahitajika uvumilivu wa hali ya juu kama aliokuwa nao Bahlul.

3.  Uislamu sahihi ni upendo na unapenda kuona wanadamu wote wanaishi kwa amani kinyume na juhudi zinazofanywa na waislamu bandia. Hivyo tuwe waislamu sahihi na wapenda amani kwa watu wote ili dunia iwe eneo salama kwa kuishi. 

Comments