KINA CHA DHATI CHA UTAKASO WA ALLAH (S.W)
KIMEFICHIKANA KWA WATU WOTE.
Sisi tuna amini ya kuwa; japokuwa athari ya
kuwepo Mwenyeezi Mungu imeenea katika ulimwengu wote, lakini uhakika wa dhati
ya Mwenyeezi Mungu ni jambo lisilo wazi kwa mwanaadamu yeyote yule, na hakuna
mtu yeyote yule anayeweza kufahamu kina cha dhati ya Mwenyeezi Mungu, kwa
sababu dhati yake Mola Mtakatifu haina mwisho, na imeizunguka kila kitu na sisi
wanaadamu tuna mipaka maalumu, mipaka ambayo ina mwisho wake, na ni kwa sababu
hiyo basi, sisi hatuwezi kuifikia dhati yake.
Ama wao wamo katika
shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Ama hakika Yeye amekizunguka kila kitu.6
Na Mwenyezi Mungu
nyuma yao amewazunguka.7
Katika hadithi maarufu ya Mtume Muhammad
(s.a.w.w) tunasoma, ya kuwa Nabii Muhammad (s.a.w.w) amesema:-
Kwa hakika sisi hatujakuabudu Wewe vile
unavyostahiki kuabudiwa, na hatujakufahamu Wewe kwa uhaki, kama vile
ilivyo haki yako kutambulika.8
Ama ni lazima tuzingatie kuwa; kauli hiyo
haimaanishi kuwa kwa sababu hatuna elimu ya kuufahamu udhati wa ndani wa Mwenyeezi
Mungu, basi vile vile hatuna elimu ya kumfahamu Mwenyeezi Mungu kijumla jamala,
kwa hakika jambo hilo halikubaliki, kwa sababu Mwenyeezi Mungu ameviteremsha
vitabu vyake ili kuwaletea wanaadamu elimu ya kumtambua Mola wao, na kwa
kupitia vitabu hivyo wanaadamu huongoka na kufikia katika saada, tunaweza
tukaashiria vitabu vingi kuhusiana na kauli hiyo, kwa mfano, sisi hatufahamu
uhakika wa roho, ama kwa upande mwingine tuna elimu ya jumla jamala
inayotuthibitishia kuwa roho ipo na tunaishuhudia.
REJEA:
[6] Surat Fussilat Aya ya 54
[7] Suratul-Buruuj Aya ya 20
[8] Buharul-Anwar, juzuu ya 68,uk23.
Comments
Post a Comment