KUFUNGWA
MILANGO YA NYUMBA ZA MASAHABA
Nasai ametoa
katika kitabu chake Khasais fi Fadhail Ali bin Abi Talib, hadith iliyopokelewa
na Zaid bin Arqam kwamba milango ya baadhi ya nyumba za masahaba ilikuwa
ikifungukia ndani ya msikiti (yaani wakitoka nyumbani mwao na kuingia msikitini
moja kwa moja) Masjid Nabi.
Mtume (s.a.w.w)
alitoa amri milango yote ifungwe isipokuwa mlango wa imam Ally (a.s). Masahaba
wakaonyesha uchungu na kutoridhika kwa amri hii. Ndipo Mtume (s.a.w.w)
akasimama na kuwahutubia. Baada ya kumsifu Mola akasema, “kwa Mujibu wa amri ya
Mwenyezi Mungu nilikuamrisheni kuifunga milango yenu na Ali aiweke wazi; hoja
na mabishano yenu hayatakiwi. Sikufunga wala kufungua mlango wa mtu yeyote kwa
hiari yangu, bali nilifuata kama nilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu.
MFUNZO;
Hii hadith
inatufundisha kuwa ubishi dhidi ya mafundisho na amri za Mtume hazikuanza leo,
bali tokea enzi za masahaba, baadhi yao walikuwa wakimbishia Mtume bila kuona
haya. Hivyo basi tujiepushe kuwafuata masahaba wabishi tusije kuangamia.
Pili tunajifunza
kuwa Imam Ally (a.s) alikuwa na cheo maalumu kwa Allah na Mtume wake. Hakuna sahaba
yeyote aliyefikia heshima na cheo alichopewa Imam Ally. Wote wanaojipandisha
cheo juu ya imam Ally ni wapotoshaji na wamo katika kundi la wabishi waliokuwa
wakimbishia mtume kila alipotoa amri hususani kuhusu uongozi wa Imam Ally (a.s).
Tatu: tufanye
juhudi ili tuwe pamoja na Imam Ally (a.s) kwani hadith hii inaonyesha kuwa
alikuwa amekwisha ridhiwa na Allah na hivyo tukimfuata yeye tutakuwa tumefuata
njia sahihi. Na kumpinga ni sawa na kuingia katika lile kundi la wabishi.
Comments
Post a Comment