KUTANGAZWA KWA SURA YA BARA’AT

KUTANGAZWA KWA SURA YA BARA’AT
Nasai anahadithia kwamba Anas amesema hivi, “Mtume (s.a.w.w) alimpeleka Abubakar kuwafikishia watu wa Maka baadhi ya aya za Mwanzo za sura ya Bara’at (sura ya 9) baadaye akamrejesha kabla hajafika na akasema, hakuna Mtu mwingine yeyote awezaye kuhubiri sura hii, isipokuwa mtu anayetokana na nyumba yangu. Basi akamwita Ali (a.s) na akamtaka ile sura ijulikanayo kama Bara’at.

Imam Ally (a.s) anahadithia kuwa Mtume (s.a.w.w) alimpeleka Abubakar na sura ya Bara’at kwenda kuitangaza Makkah. Baadaye akanipeleka nyuma yake na akaniambia, “chukua kwa Abubakar maandiko ya Sura ya Bara’at na uende kwa watu wa Makkah. Hivyo nikaondoka na njiani nilimkuta Abubakar na nikayachukua maandiko.

Abubakar akarejea kwa Mtume (s.a.w.w) na huzuni, akauliza, “ewe Mtume wa Allah, je umeelekezwa na Mwenyezi Mungu juu yangu? Mtume akajibu; sivyo, bali Mola ameamuru kuwa mimi binafsi au mmoja katika watu wa nyumba yangu (Ahlulbayt) aitangaze sura ile.

Na katika hadith nyingine iliyoandikwa na Nasai na Tirmidhi, pia inasema kuwa maneno yafuatayo hapa yametumiwa na Habshi bin Janada – Mtume (s.a.w.w) alisema, isipokuwa Ali (a.s) na mimi binafsi, hakuna mtu mwingine tena awezaye kuitangaza kama inavyotakikana.

FUNZO:
Hadith hii inathibitisha ubora wa Imamu Ally juu ya masahaba wengine kwa kuwa yeye ni Ahlulbayt wa Mtume na pia anao uwezo mkubwa kielimu kuliko masahaba wengine
Pili hadith hii inaonyesha kuwa Imam Ally (a.w) alikuwa kama waziri wa Mtume (s.a.w.w) kwa sababu mambo mazito yalitangazwa na Mtume mwenyewe au imamu Ally pekee.
Tatu hadith hii inatufundisha kuwa Abubakar sio Ahlulbayt kama watu wengine wanavyodai na wala hakuwa na ubora wowote wa kuwazidi masahaba wengine (kwa mfano Imam Ally, Zaidi bin Harith, Ammar bin Yasir, Abudhar bin Ghiffar, Salman Farsi, Usama bin Zaidi na wengine wengi).

Safari nyingine tutaeleza ubora wa sahaba mmoja mmoja na sio kama baadhi ya watu wanaotudanganya kuwa masahaba bora ni watatu tu yaani Abubakar, Umar na Uthuman. Ukweli ni kinyume cha hayo,

Comments