KUTHIBITISHA RISALA (UJUMBE) NA WAHYI WA MTUME MUHAMMAD (S.A.W).

KUTHIBITISHA RISALA (UJUMBE) NA WAHYI WA MTUME MUHAMMAD (S.A.W).
Mtume Muhammad (s.a.w) ni mtu aliyekuwa hakusoma, na hakuonekana kukaa na watu Maulamaa, lakini jambo lililowashangaza baadhi ya watu ni kwamba Mtume huyo alikuwa akiwatolea watu simulizi na historia zinazohusiana na Mitume waliopita, kwa mfano, historia ya Nabii Ibrahimu, Yussuf, Mussa, na Issa (a.s), mtu ambaye hakusoma wala hakuwa na elimu yoyote ni muhali kujua habari muhimu (historia), kama hizo. Kwa hiyo historia kama hizo zilizomo ndani ya Qur-an ni zenye kustaajabisha na kuleta maajabu, na hiyo basi ni dalili kubwa ya kuthibitisha wahyi na ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w).

Qur-ani pia inathibitisha hayo katika Surat Yussuf Aya ya 2-3, pale Allah (s.w) anaposema:- Hakika sisi tumeiteremsha Qur-an kwa Kiarabu ili mpate kufahamu.
Sisi tunakusimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur-an hii, na hakika ulikuwa kabla ya haya ni miongoni mwa wasio na habari (hizi).
Aya hizo zinatilia mkazo na kusisitiza kuwa (Mtume Muhammad (s.a.w) hakuwa na habari yoyote kuhusiana na simulizi hizo, na Mwenyeezi Mungu alimjulisha na kumpa habari hizo kwa njia ya Wahyi. Hii basi ndio dalili ya kuthibitisha kuwepo kwa Wahyi.

Kwa hiyo ujuzi na elimu yote aliyokuwa nayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) alivipata moja kwa moja toka kwa Mwenyezi Mungu na hakuna Mtu anayeweza kusema kuwa Mtume alikuwa mwanafunzi wake. 

Comments