MADHAMBI YAMFANYAYO MTU KUINGIA
JAHANNAM
Mwanadamu yupo daima anatenda madhambi kutokana na nafsi yake mwenyewe.
Malaika walipomwabia Allah (sw) kuwa mjumbe wake huyu atakuwa mtenda madhambi.
Naye Allah (sw) akawaabia kuwa yeye ayajua zaidi kuliko wao.
1. Mtu kuchuma
mali na kurundika
Mtu yule ambaye atakusanya fedha na kuziweka mahala pamoja bila ya
kufaidika yeye wala kuwasaidia wengineo ambapo wapo ndugu zake Waislamu wenye
shida ambapo maisha yao yamewawia magumu. Mtume s.a.w.w. amesema kuwa "ufukara
ni mbaya zaidi ya ukafiri". Vile vile Imam Ali a.s. amesema Daima mchunge
kuwa mwenye "shida masikini asikuijie bali ni wajibu wako wewe
uwafikie."
2.
Mwanadamu hufikia wakati wa kukufuru ama kwa kukusudia
au bila kukusudia. Siku moja mtu mmoja alikuwa akisafiri kwenda mji mwingine
kwa ndege. Ndugu yake ambaye alikuwa akimsindikiza uwanjani hapo alimwuliza
"Ewe ndugu yangu! Je hautakuwa na shida ya fedha wakati ukiwa safarini?"
Ndugu yake ambaye alikuwa akisafiri alimjibu "Naam Ndugu yangu! Mimi sitakuwa
muhitaji wa Allah (sw) kwa muda wa juma moja hivi." Ndege iliruka na
katika muda wa nusu saa hivi kulipatikana habari kuwa ndege hiyo imeanguka na
wasafiri wote wameuawa.
Hapa siwezi kusema kuwa watu wote hao wamekufa kwa sababu ya kuadhibiwa
mtu mmoja aliyetoa maneno ya kashfa dhidi ya Allah (sw). Na kwa maana hii ndipo
tunapoambiwa kuwa sisi tusijihusishe na mahala ambapo panapotendeka maasi na
madhambi kwa sababu inawezekana adhabu za Allah (sw) zikateremshwa hapo na wewe
ukakumbwa pamoja humo.
3. Kuwadhalilisha
waja wa Allah wawe wazima au wamekufa.
Kisa cha kijana mwenye madhambi
Ma'adh anasema: "Siku moja nilikuwa nikijiandaa kwenda kwa Mtume (s.a.w.w.),
na mara nikamwona kijana mmoja akilia mno, basi hapo nilimwuliza sababu ya
kilio chake hicho. Huyo kijana alinijibu kuwa yeye ni mwenye dhambi kubwa mno.
Basi hapo nilimwambia aje pamoja nami kwa Mtume (s.a.w.w.) ili amwombee msamaha
kwa Allah (sw). Hapo huyo kijana alisema kuwa alikuwa akiona aibu kuja mbele ya
Mtume s.a.w.w. kwa sababu ya dhambi zake."
Hapo Ma'adh aliendelea na safari yake hadi kwa Mtume (s.a.w.w.) na
kumwelezea yale yaliyotokea. Basi Mtume (s.a.w.w.) alimwambia akamlete yule
kijana. Alipofika mbele ya Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa, 'Je umekuwaje, walia kwa
nini? Hapo huyo kijana akasema, "Ewe Mtume wa Allah sw! Dhambi yangu ni
kubwa mno!" Hapo Mtume (s.a.w.w.) aliendelea kumwuliza, "Je kosa lako
kubwa au mbingu?" Akajibu, 'Kosa langu!' 'Je kubwa au dunia nzima?
Akajibu, kosa langu! Je kosa lako kubwa au msamaha wake Allah (sw)? Hapo huyo
kijana akasita na hatimaye kukubali kuwa 'Msamaha wa Allah (swt) ni mkubwa! Basi
hapo Mtume alimwuliza, sasa niambie kosa lako.
Huyo kijana akaanza kusema: "Ewe Mtume wa Allah swt! Palitokea
kufariki kwa binti mmoja mzuri mno wa kabila la ansaar, na mimi nilikwenda
usiku ule kulifukua kaburi ili kutaka kuiba sanda aliyokuwa amevishwa huyo
maiti, shetani alinighalibu na kunifanya nikatenda tendo la kinyama kwa maiti
huyo, binti aliyekuwa uchi mbele yangu. Hapo ndipo maiti hiyo ilipotoa sauti ya
masikitiko na kunilaani kwa kuniambia kuwa Allah sw ataniingiza motoni na kuniunguza
humo kuteketea. Ewe mtume wa Allah sw kwa hakika, baada ya matamshi hayo ya
maiti huyo, mimi nimekosa furaha ya kila aina na nimeingiwa na woga na nadhani
nitaweza kuangamia katika hali kama hii iwapo itaendelea kunisumbua. Hapo mtume
s.a.w.w. alimwambia huyo kijana: "Ondoka haraka mbele yangu kwani
inawezekana moto wa Jahannam ukanikumba nami pia." Je kwa nini Mtume
alisema hivyo? kwa sababu dhambi lilikuwa kubwa mno!
Kwa mujibu wa riwaya, kijana huyo baada ya kuambiwa hivyo, aliondoka akiwa
amesikitika mno na kuelekea katika milima ya mji wa madina, huko alikaa kwa
muda wa siku arobaini akiwa akilia na kuomba Toba kwa Allah sw. Baada ya siku
arobaini kupita, alisema: "Ewe Allah sw! Iwapo umeshakwisha kuikubalia
Toba yangu, basi naomba unijulishe kwa kupitia Mtume wako. Na iwapo bado
haujaikubali Toba yangu, basi naomba uniteremshie miale ya moto kutoka mbinguni
ili inichome na kuniunguza ili niteketee kabisa!"
Basi hapo iliteremka Aya ya 134 - 135 ya sura Ali
Imraan:
"Na wale ambao, wanapofanya tendo la kuaibisha au kudhulumu nafsi
zao, wakamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani
awasamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu? Na ambao hawabakii (kwa kukusudia)
katika yale waliyoyafanya maovu hali walikuwa wakiyajua hayo."
Comments
Post a Comment