MASHIA NI AKINA NANI,AU NINI MAANA YA SHIA?:
Shia ni jina amabalo huitwa wale watu wa dhehebu la pili la waislaam kwa ukubwa,nao ni wale ambao hujulikana kihistoria kama "شيعة علي"= SHIAT ALI= "MASHIA WA ALI" yaani (wafuasi wa Ali) au "أتباع علي"= (Wafuasi wa Ali).

Na mara nyingi Istilahi hii inapotajwa huashiria MASHIA AMBAO NI WAFUASI WA MAIMAM KUMI NA WAWILI,na katika Mashia hili ndilo kundi kubwa zaidi ukilinganisha na mashia wengine ambao si wafuasi wa Maimam Kumi na wawili kama mashia wale wanaoitwa Zaidiyya,na Ismailiyya hawa pia ni Mashia lakini si mashia wenye kufuata Maimam Kumi na wawili bali ni mashia ambao wanaishia kwa Zaidi na Ismaili na ndio maana wakanasibishwa kwa majna hayo wakaitwa Zaidiyya na Ismailiyya.
Hivyo tunaposema Mashia hatumaanishi au kukusudia Mashia Zaidiyya wala Mashia Ismailiyya, bali tunamaanisha wale Wafuasi (Mashia) ambao hufuata Maimamu Maasumini Kumi na wawili kutoka katika Kizazi Kitukufu cha Mtume (s.a.w.w) na ambao ndio walioteuliwa na Mtume (s.a.w.w) kuwa Makhalifa na Mawasii baada yake kwa dalili zilizowazi ndani ya vitabu vya kishia na kisunni.
Hivyo: Mashia hawa au wafuasi hawa kwa kuwa wanafuata Maimam 12 wa Ahlul-bait (a.s) ndio maana wakaitwa SHIA ITHNA ASHARI, kwa maana MASHIA au WAFUASI WENYE KUWAFUATA MAIMAM KUMI NA WAWILI. Na Maimam hao kumi na wawili (12) watwaharifu (a.s) majina yao yametajwa katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w) na riwaya mbalimbali zilizopokelewa kwa pande zote mbili au kwa Madhehebu zote mbili yaani: Shia Ithna Ashari na Ahlu Sunna.
Na hivyo hivyo kuhusu Shia, ukisema shia unaeleweka umesema Shia, lakini hueleweki umekusudia shia wepi hivyo ni bora useme Shia zaidiyya au Shia Ismailiyya au Shia Ithna Ashari.
Maana hizi zinapatikana maeneo mengi hata ukiangalia katika kamusi utapata maelezo haya. Hivyo hapa hitaji rejea.
Maana hizi zinapatikana maeneo mengi hata ukiangalia katika kamusi utapata maelezo haya. Hivyo hapa hitaji rejea.
Comments
Post a Comment