MASHIA WALIMU WA AHLUL-SUNNAH WALJAMAA

MASHIA WALIMU WA AHLUL-SUNNAH WALJAMAA
Imam Maliki anasema, ‘ jicho halijaona wa sikio halijasikia, wala halijapita wazo katika moyo wa mtu yeyote (kuwa kuna) mbora kuliko Imam Jaafar Assadiq kwa utukufu, elimu, ibada na ucha Mungu’.

Imam Abu Hanifah anasema, “Lau si miaka miwili, basi Nuu’man angeangamia” akiwa anakusudia miaka miwili aliyosoma kwa Imam Jaafar Assadiq (a.s).
Tazama: kitabu Manaqib Ali bin Abi Talib, kuhusu mazingira ya imam Ja’far As-Sadiq.


Maimamu wa Ahlu-Sunnah wanamsifia na kumwona kuwa ni mkombozi wao Imam Jaafar As-Sadiq. Je ni nani huyo? Imam Jaafar As-Sadiq ni Imam wa sita wa waislamu kwa kuteuliwa na Mtume (s.a.w.w), wa kwanza wa maimamu hao ni Imam Ally na wa mwisho wao ni imamu Mahdi. Hao ndio maimamu wanafuatwa na Mashia Ithnashariyyah, na kuwaamini kuwa ni maasumu na wasio tenda dhambi na waliowafanyia uadui ni waovu na waliopupia madaraka yasio kuwa yao.

Comments