MATAWI YA DINI (UISLAMU):

MATAWI YA DINI (UISLAMU):
Matawi ya dini ni hukumu alizoziweka Allah Mtukufu kupitia Qur’an na Sunna tukufu kwa maslahi ya waja wake, na ambazo Mtume (s.a.w.w.) ametulingania kuzifuata, na akatuamuru kuzitekeleza, zikiwa na lengo la kuzitoharisha nafsi na kuimarisha utumishi wake kwa Allah Mtukufu.

Matawi ya dini yaliyo muhimu zaidi ni:
1. Swala
2. Saumu
3. Zaka
4. Hijja
5. Khumsi
6. Jihad (kufanya juhudi katika dini)
7. Kuamrisha mema na kukataza maovu
8. Kumtawalisha Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayti wake watoharifu
(a.s) na kujiepusha na adui zao.


Kila mwislamu lazima atekeleze haya kama kweli anataka kupata radhi za Muumba. Maelezo ya kila kimoja yatafuatia insha-Allah.

Comments