MITUME WOTE WALIKUJA KUWAALIKA WATU KUMTII MWENYEEZI MUNGU MMOJA.

MITUME WOTE WALIKUJA KUWAALIKA WATU KUMTII MWENYEEZI MUNGU MMOJA.
Mitume wote walioletwa na Mwenyeezi Mungu walikuja na madhumuni moja, nalo ni kumuongoza mwanaadamu katika njia moja, nayo ni kumuabudu Mola mmoja. Na Mitume wote walifikia katika kusudio moja na sio zaidi ya hapo.
Vile vile kulikuwa kuna watu ambao walikuwa wakikabiliana na Mitume na kuyapinga yale ambayo wanayaamrisha, watu hao vile vile walisimama kidete kwa kutumia njia moja ili kufikia katika makusudio yao. (ili kupata ufafanuzi zaidi rejea kitabu cha Elimu ya Qur-ani, Intisharati simat wa tamhiydiy, ukurasa wa 278).


 Lazima tujiulize kama mitume wote ujumbe wao ulikuwa mmoja, nani sasa kaleta dini nyingi? Au ni nani basi kaleta madhehebu mengi? Bila shaka hiyo ni kazi ya shetani. Ni lazima tufanya juhudi za makusudi kuzichunguza dini zetu na madhehebu zetu ili kubaini kama ni za kweli au za uongo (bandia). Tutakapogundua kuwa dini zetu au madhehebu zetu ni bandia basi tuzihame mara moja na kuufuata ukweli. 

Comments