MIZIZI YA DINI YA KIISLAMU:
Dini ni mkusanyiko wa imani na majukumu ya kivitendo
yaliyoletwa na
Manabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili kuwaelekeza na
kuwaongoza
wanadamu. Hivyo nafsi kujengeka katika msingi wa imani
hizi huku
ikitekeleza majukumu haya ya kivitendo ndiyo sababu ya
mwanadamu
kufanikiwa kwa wema ndani ya maisha haya ya Dunia na
Akhera, hivyo
mizizi hiyo ya dini ni mitano:
i. Tawhidi:
Ni kuamini kuwa ulimwengu una Mungu aliyeuumba na kuufanya uwepo baada ya kuwa
haukuwapo, na kwamba huyo
Muumba wa ulimwengu ni Mmoja Mpekee asiyekuwa na mshirika.
ii.Uadilifu:
Ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mwadilifu, hamdhulumu yeyote, na
kwamba matendo Yake yana hekima, hivyo, hatendi chochote isipokuwa kina
masilahi kwa viumbe.
iii. Utume:
Ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu hawaachi viumbe wake bila mwongozo, hivyo
aliwatuma manabii ili wawaite watu kwenye njia iliyonyooka. Na Nabii wa kwanza
ni Nabii Adam (a.s) na wa mwisho ni Nabii Muhammad (s.a.w.w), na kwamba dini
ikubaliwayo kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu na ndio dini kamili.
iv. Uimamu:
Ni kuamini kuwa, kama ambavyo Mwenyezi Mungu aliteua Manabii na mitume,
vivyo hivyo aliteua warithi wa Mitume
wake. Ili kuendeleza kazi ya unabii wa bwana wetu Muhammad
(s.a.w.w.) aliwateua Maimamu, warithi na Makhalifa kumi na wawili, wa kwanza
wao ni Ali bin Abi Twalib (a.s) na wa mwisho ni Imam Al-Mahdi (a.t.f.s).
v. Marejeo:
Ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawafufua watu baada ya kifo ili
kumlipa mtiifu kwa wema na kumwadhibu aliyeasi, ili awape malipo ya kudumu.
Allah akipenda tutafafanua kila mzizi kivyake ili kuleta uelewa mpana wa
dini yetu, katika mada zijazo.
Comments
Post a Comment