MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) NDIYE WA MWISHO

MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) NDIYE WA MWISHO
Sisi Mashia tuna itakidi ya kuwa; Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndiye Mtume wa mwisho wa Mwenyeezi Mungu, na sheria na malinganio yake ni kwa ajili ya watu wote duniani, na sheria hizo zitabakia milele hadi mwisho wa dunia, kauli hiyo inathibitisha kuwa taaluma na hukumu zote za dini ya Kiislamu zinakidhi na kudhamini mahitajio yote ya wanaadamu, ya duniani na Akhera hadi mwisho wa dunia, kwa hiyo, mtu yeyote yule atakayekuja na madai ya kuwa yeye ni Mtume, basi madai hayo si ya kweli na yatakuwa hayana msingi wowote kwa wanaadamu.

Allah anasema katika Qur’an takatifu, “Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu”.

Hii ndio itikadi yetu na anayedai kinyume na hayo dhidi yetu basi ni mwongo anayeeneza imani yake kwa kutuzulia uongo sisi. Hakika imani inayoenezwa kwa uongo hiyo sio dini sahihi bali itakuwa na ushetani ndani yake.

Kwa hiyo wale wote wanaotusingizia uongo sisi Mashia ni mashetani waliojiingiza katika Uislamu ili kuwapotosha waumini. Haiwezekani wao waujue Ushia (Uislamu) kuliko sisi wenye imani yao.

Comments