MUBAHALA (MAAPIZANO
KATI YA MTUME NA WAKRISTO)
Kabla hatujaingia ndani kuzungumzia suala la Mubahala, kwanza ni vizuri tufahamishe maana ya Mubahala. Muhabala ni: Kuapizana. Ujumbe wa Kikristo kutoka Najran ulifika kwa Mtume kujadili suala la Nabii Isa (a.s.). Mtume aliwajulisha kuwa: Hakika mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa. (3:59).

Kwa kuwa
Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi
Mungu. Aya hii inaondoa dhana hiyo ambayo inapingana na utukufu wa Mwenyezi
Mungu, na inawapigia mfano wa ajabu zaidi katika kuumbwa Adam bila ya baba wala
mama. Aliumbwa kwa udongo kisha akaambiwa: kuwa naye akawa, na kwa neno hilo
hilo Nabii Isa (a.s) ndivyo alivyoumbwa.
Ujumbe huo
ulipokuwa haukukubaliana na hoja hii, Mwenyezi Mungu akateremsha Aya:- "Na
atakayehojiana nawe (Muhammad) katika hili baada ya ujuzi uliokufikia, waambie:
Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu,
na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa kunyenyekea tuijaalie laana ya
Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo." (3:61).
Hili lilikuwa
tarehe ishirini na nne mfungo tatu mwaka wa kumi. Mtume akawaita ili waanze
kuapizana. Wakajibu:- "Ngojea tujadiliane". Walipokwenda faragha,
wakamuuliza Askofu Abdul Masih; ana Maoni gani katika suala hili? Akajibu:-
Enyi Wakristo: Wallahi nyinyi mnajua kuwa Muhammad ni Nabii aliyeletwa na
amekuja na ushahidi ulio wazi juu ya jambo la huyu (Yesu a.s.). Wallahi hakuna
watu walioapizana na Nabii wakasalimika, ikiwa mtaapizana naye
mtaangamia".
Askofu Peter
yeye aliwaambia: "Enyi Wakristo: Mimi naziona nyuso hizi (kundi la Mtume)
kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, Wallahi
atauondoa. Msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki Mkristo ye yote hapa duniani
mpaka siku ya Kiama".
Alipoulizwa Ahtam, akawaambia: Niacheni nikamuulize Muhammad, alipomkabili Mtume akamuuliza, "Ewe Abulqasim'! Unatoka na kina nani kwa ajili ya maapizano haya?" Mtume (s.a.w.) akamjibu: "Ninaapizana nanyi nikiwa na watu bora hapa duniani na watukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu, nao ni hawa (akawaonyesha) Ali, Fatima, Hasan na Husein."

Taarifa ya
kikosi hicho cha Mtume (s.a.w) ilipowafikia wakaogopa kuapizana na Mtume, na
badala yake wakaomba sulhu kwa Mtume (s.a.w.) kwa kutoa dirham arobaini elfu.
TAZAMA:
Tarikh Ibn
Athir J.2 Uk. 200
Tafsirul
Qurtubi J.4 Uk. 104
Tafsirul Ibn
Kathir J.1 Uk. 376-379
Tafsirul
Khazin J.1 Uk. 359-360
Tafsirul
Maragh J.3 Uk. 175
Tafsirul
Kabir J.8 Uk. 81
Zadul Masir
J.1 UK. 399
Katika Ayatul Mubahala, iliposema:- "Tuwaite watoto wetu" Mtume (s.a.w.) alimwita: Hasan na Husein. Iliposema: "Na wanawake wetu" Mtume (s.a.w.) alimwita: "Fatima bint Muhammad". Iliposema: "Na nafsi zetu" mtume akamwita: "Ali". Kwa hivyo Ali bin Abi Talib ni nafsi ya Mtume Muhamad (s.a.w.).

Tukio hili
Ia Mubahala tukilitazama kwa upande wa pili, linatukumbusha lile tukio la
"KlSAA" Iliposhuka Ayatut Tat'hir:- Hakika Mwenyezi Mungu anataka
kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana
sana" (33:33). Iliposhuka Aya hii Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan
na Husein, akawafunika nguo kisha akasema: "Ee Mola! Hawa ni watu wa
nyumba yangu, basi waondolee uchafu na uwatakase sana sana." Mama Ummu Salama
(mke wa Mtume) alipotaka kuingia humo, Mtume (s.a.w.) akamzuia:
Kama ambavyo
kwenye tukio la Mubahala ulipofika wakati wa kuomba maombi maalumu kwa ajili ya
maapizano kati yake na Wakristo wa Najran, Mtume alimchukua Ali na Fatima na
Hasan na Husein tu. Ingawa wakati huo Mtume (s.a.w.) alikuwa nao wakeze, na
Masahaba ambao ni marafiki zake pia, lakini hapa hawakuingia. Wake za Mtume na
Masahaba hawakuingia katika "KISAA" na hawakusimama katika uwanja wa
Mubahala, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwahusisha darja hii Ahlul Bait tu peke
yao.
TAZAMA:
Tafsirul
Khazin J.3 Uk. 259
Tafsirul Ibn
Kathir J.3 Uk. 494
Tafsirul
Qurtubi J.14 Uk. 183
Zadul Masir
J.6 Uk. 381
Comments
Post a Comment